IQNA

Waislamu nchini Nigeria

Mashindano ya Kila Mwaka ya Kuhifadhi Qur'ani Yafunguliwa Zamfara , Nigeria

15:12 - December 17, 2022
Habari ID: 3476259
TEHRAN (IQNA) - Gavana wa Jimbo la Borno la Nigeria Ijumaa alitangaza ufunguzi wa mashindano ya kila mwaka ya kuhifadhi Qur'ani yaliyoandaliwa na Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu cha Chuo Kikuu cha Usman Dan Fodio.

Babagana Umara Zulum, ambaye ni mwenyekiti wa hafla hiyo, alizitaja juhudi za Mkuu wa Jimbo la Zamfara katika kuandaa mashindano ya mwaka huu licha ya matatizo ya kiuchumi, kuwa ni jambo la kupongezwa sana.

Zulum alisifu fadhila nzuri za Gavana Matawalle ambaye alisema anastahili cheo anachobeba, cha "Khadimul Qur'ani" (mtumishi wa Qur'ani Tukufu).

"Msukumo mkubwa wa kuvumilia juhudi zinazofanywa kukuza Qur'ani Tukufu miongoni mwa vijana ni dalili kwamba dhamira ya gavana wa jimbo kwa serikali na wananchi wa Jimbo la Zamfara ilikuwa kwa ajili ya ustawi wa jamii," alisema.

Ameongeza kuwa, maelfu ya changamoto zinazoikabili Nigeria leo zinaweza kupunguzwa iwapo wananchi watakubali mafundisho ya Qur'ani Tukufu. Baadaye alitoa kiasi cha N10 milioni kwa ajili ya kufanikisha tukio hilo la wiki nzima.

Katika hotuba yake akiwa mwenyeji mkuu wa hafla hiyo, Gavana Matawalle alielezea umuhimu wa mashindano hayo ambayo alisema ni pamoja na kutafsiri maneno ya Mwenyezi Mungu kwa vitendo.

Amesema umuhimu wa Qur'ani Tukufu katika maisha ya Waislamu na muongozo unaoutumikia ndio mambo makuu anayopaswa kuyatarajia kutokana na mwenendo wa tukio hilo na baada ya hapo.

Awali, Naibu Gavana wa Jimbo la Zamfara, Seneta Hassan Mohammed Gusau alisema mashindano hayo yalifanikiwa kwa uungwaji mkono kamili wa Gavana Bello Mohammed.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Usman Dan Fodio, Profesa Bilbis aliipongeza serikali ya Jimbo la Zamfara kwa kuandaa mashindano ya mwaka huu ambayo alisema ni kielelezo cha utayari wa Jimbo hilo kuendelea kuinua hadhi ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Alitoa wito kwa washindani kuzingatia ushiriki wao kama mchango katika kukuza utamaduni  wa Qur'ani Tukufu.

Naye Mgeni Rasmi, Sheikh Ibrahim Ahmad Maqari, alizungumzia haja ya kulinda vituo vya masomo ya Qur'ani kote katika jamii za Kiislamu nchini Nigeria. Profesa Maqari pia alitetea uidhinishaji mtaala wa kisasa wa vituo vya Qur'ani visivyo rasmi vilivyoenea katika jamii  Kiislamu kote Nigeria.

3481702

Kishikizo: nigeria waislamu zamfara
captcha