IQNA

Waislamu Ujerumani

Maiti ya Muislamu yachomwa moto ‘kimakosa’ Ujerumani

21:58 - December 23, 2022
Habari ID: 3476294
TEHRAN (IQNA) – Maiti ya Muislamu mmoja ilichomwa moto nchini Ujerumani baada ya hospitali mjini Hannover kuchanganya maiti mbili.

Abdulkadir Sargin, raia wa Uturuki, alifariki katika huduma ya dharura ya Hospitali ya Shule ya Matibabu ya Hannover wiki iliyopita, maafisa wamesema.

Wakati wa maandalizi ya mazishi siku ya Jumanne, wanafamilia wa Sargin walishtuka na kuchanganyikiwa walipoona mtu aliyekuwa kwenye jeneza alikuwa mwingine.

Walipopigia simu hospitalini, walifahamishwa kuwa wafanyakazi hao waliukabidhi mwili wake kwa familia nyingine kimakosa na kwamba tayari maiti ilikuwa imeshachomwa moto.

Uchomaji moto maiti ni haramu katika sheria za Kiislamu na kitendo hicho huhesabiwa kuwa ni sawa na kumvunjia heshima marehemu.

Ubalozi mdogo wa Uturuki mjini Hannover unawasiliana kwa karibu na wanafamilia hao na utatoa msaada unaohitajika kwao, maafisa wamesema.

3481791

captcha