IQNA

Kumbukizi ya Shahidi Soleimani

Jihad Islami:Shahidi Soleimani aliweza kuwapa motisha wapiganaji wote wa mrengo wa Muqawama

20:36 - January 03, 2023
Habari ID: 3476351
TEHRAN (IQNA) – Mwanachama mwandamizi wa harakati ya muqawama au mapambano ya Palestina, Jihad Islami, amesema shahidi Qassem Soleimani aliweza kutoa motisha kwa wapiganaji wote wa harakati za mapamano.

Yusuf al-Hassayina alisema hayo alipokuwa akihutubia kwenye warsha ya kimataifa kwenye intaneti kuhusu Fikra za Shahidi Soleimani.

Warsha hiyo ya mtandaoni ilifanyika Jumanne asubuhi na kusimamiwa na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA)  lenye makao yake katika mji mkuu mkuu wa Iran, Tehran ambao anuani ya warsha hiyo ilikuwa ni  "Hadhi, Usalama na Uhuru katika Fikra za Shahidi Soleimani".

Lt. Jenerali Soleimani, ambaye alikuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Naibu Kamanda Jeshi la Kujitolea la Wannachi wa Iraq (PMU) Abu Mahdi al-Muhandis, na wanamapambano wenzao waliuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mapema  Januari 3, 2020. Shahidi Soleimani alikuwa ameelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa serikali ya nchi hiyo.

Ikulu ya White House na Pentagon ilitangaza kuwa ilihusika na mauaji hayo ya kigaidi  na kuthibitisha kuwa shambulio hilo lilitekelezwa kwa maelekezo ya Rais wa Marekani wa wakati huo Donald Trump.

Akihutubu katika warsha hiyo,  ya mtandaoni au webinar, Hassayina alisema kwamba Shahidi Soleimani alikuwa mfano wa kipekee katika uongozi wa kijeshi na kujitolea mhanga, na kuongeza kuwa vuguvugu la mapambano au muqawama nchini Palestina lilishuhudia maendeleo ya msingi kutokana na kujitolea mhanga na Jihad ya Luteni Jenerali Soleimani.

Amesema kwa uungaji mkono wa Iran, Jenerali Soleimani, na IRGC, na miongozo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei, nguvu ya muqawama inaongezeka na kuwafanya maadui kutetemeka.

Afisa huyo wa Harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina pia amesema Mashahidi Soleimani na al-Muhandis walianisha  njia yao katika nyuga za muqawama na Jihad, ambayo ni njia ya adhama, ushindi na heshima na hivyo urithi wao huo utaendelea.

Damu safi ya mashahidi hao wawili itaendelea kutoa msukumo wa muqawama ili kuendelea na ushindi, alisema, akisisitiza kuwa Palestina na taifa la Palestina kamwe hazitasahau kujitolea mhanga na ushujaa wa mashujaa hao wawili.

Hassayina pia amemnukuu Ayatullah Khamenei akisema kwamba kutokana na damu ya Shahidi Soleimani, harakati ya muqawama ina furaha na matumaini zaidi hivi leo.

Aliomba baraka za Mwenyezi Mungu kwa ajili ya roho za mashahidi na nguvu kwa ajili ya Jamhuri ya Kiislamu na mbele ya mapambano.

Wazungumzaji wengine kwenye warsha hiyo ya mtandaoni walikuwa ni pamoja na mjumbe wa Baraza la Walinzi wa Katiba la Iran Ayatullah Seyed Ahmad Hosseini Khorasani, mwanazuoni wa Chuo Kikuu cha Damascus Bassam Abu Abdullah, na Sayed Hussein al-Bakhati, afisa wa Jeshi la Kujitolea la Wannachi wa Iraq (PMU).

Hassan Pelarak, mmoja wa wapiganaji wenza wa Shahidi Soleimani, alitoa hotuba katika Studio ya IQNA ya Mobin huku wazungumzaji wengine wakihutubia semina hiyo kupitia video.

Fikra za Shahidi Soleimani na Kadhia ya Palestina, Fikra za Shahidi Soleimani na Hotuba za Muqawama, Fikra za Shahidi Soleimani na Mustakabali wa Mfumo wa Ubeberu, na Usalama wa Kijamii Katika Mawazo ya Shahidi Soleimani, zilikuwa baadhi ya mada zitakazojadiliwa kwenye  warsha hiyo.

4111185

captcha