IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu /15

Msisitizo wa Maurice Bucaille juu ya uhusiano kati ya sayansi na dini

16:06 - January 04, 2023
Habari ID: 3476354
TEHRAN (IQNA) – Maurice Bucaille alikuwa tabibu Mfaransa aliyesoma Qur'ani Tukufu na vitabu vingine vya Mwenyezi Mungu na akaamini kwamba kuna uhusiano kati ya sayansi na dini. Vile vile alirejea kwenye miujiza ya kisayansi ya Qur'ani Tukufu ambapo alisisitiza kuhusu asili ya kitabu hicho kitakatifu.

Suala la muujiza wa kisayansi wa Qur'ani Tukufu lilitajwa kwa mara ya kwanza na mwanachuoni na mtafiti wa Misri Abd al-Razzaq Nawfal.

Majadiliano kuhusu mada hii yalizidi kuwa ya kina katika miaka ya 1950 na daktari Mfaransa Mkatoliki Maurice Bucaille, ambaye alipendezwa na Utaalamu Historia ya Misri (Egyptology) na kusoma hieroglyph na alijiunga na jamii ya Egyptology nchini Ufaransa.

Bucaille pia alikuwa daktari maalum wa Mfalme Faisal wa Saudi Arabia na alikuwa karibu na ulimwengu wa Kiarabu. Alizungumza Kiarabu na kuandika kitabu kiitwacho “Quran, Torati na Biblia; Utafiti Katika Nuru ya Sayansi ya Kisasa” ambao unachukuliwa kuwa hatua ya mabadiliko katika masomo ya miujiza ya Qur'ani Tukufu.

Kitabu hiki kilitafsiriwa katika makumi ya lugha katika miaka ya 1970 na kilikaribishwa na Waislamu wengi.

Hata hivyo, ilishambuliwa na majarida ya kisayansi ambayo yaliona kuwa ni kosa kuunganisha nadharia za kisayansi na maandishi ya kidini.

Kwa hivyo Bucaille ni mwanzilishi katika uwanja wa kusoma miujiza ya kisayansi ya Quran. Mtazamo wake wa kuunganisha dini na sayansi na kitabu chake ulizua vuguvugu lililoitwa Bucailleism.

Katika kitabu “Quran, Torati na Biblia; Utafiti katika Nuru ya Sayansi ya Kisasa”, Bucaille analinganisha aya za Quran na sayansi za kisasa ili kuthibitisha asili ya imani Kiislamu na Qur'ani Tukufu.

Bucaille alizaliwa Julai 19, 1920 nchini Ufaransa na kufariki Februari 17, 1988. Aliteuliwa kuwa daktari wa familia ya Faisal wa Saudi Arabia mwaka 1973. Pia alikuwa daktari wa baadhi ya wanafamilia wa Anwar Sadat, rais wa zamani wa Misri.

Maurice Bucaille alikuwa Mkatoliki aliyeukubali Uislamu. Alisomea udaktari na kufanikiwa kuwa mmoja wa madaktari bingwa wa upasuaji.

Alikuwa mmoja wa watu mashuhuri wa mashariki wa Magharibi ambaye alidhihirisha hadhi ya Uislamu kwa nchi za Magharibi na kuthibitisha kwamba hakuna pengo kati ya sayansi na dini.

3481936

captcha