IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu /12

Uzingatiaji ubora wa kilugha katika tarjuma za Qur'ani Tukufu eneo la Balkan

20:24 - December 19, 2022
Habari ID: 3476273
TEHRAN (IQNA) – Shughuli za kutarjumi Qur'ani Tukufu imeshuhudia maendeleo makubwa katika eneo la Balkan katika miongo ya hivi karibuni.

Kumeshuhudiwa hatua kutoka wakati ambapo wasomi katika eneo walitoa tarjuma ambazo pia zilijumuisha tafsiri ya Qur'ani Tukufu hadi miaka ya hivi karibuni ambapo wamekuwa wakizingatia ubora wa fasihi katika lugha katika tarjumi.

Nukta hii humsaidia msomaji kufurahia uzuri wa maandishi ya Kitabu Kitakatifu na uzuri wa uzuri wa lugha.

Baada ya kuongezeka kwa tarjuma za Qur'ani Tukufu duniani, wasomi katika eneo la Balkan, ikiwa ni pamoja na Bosnia na Herzegovina, Albania na Kosovo, pia walipata hamu ya kufanya kazi katika uwanja huo. Kwa mfano, wanazuoni wawili wa Kiislamu huko Kosovo wanaojulikana kama Sherif Ahmeti na Hasan Nahi walitarjumi Kurani na kuchapisha tafsiri yao mnamo 1988.

Baada yao tafsiri zaidi za Qur'ani Tukufu zilichapishwa na idadi ikafikia 12.

Wafasiri na watarjumi wa kizazi kipya ambao walikuwa na ujuzi katika nyanja mbalimbali za lugha, fasihi, sheria, falsafa na uzuri, walinufaika kutokana na ujuzi wao.

Tarjuma ya kwanza ya Qur'ani Tukufu  kutoka kwa Kiarabu katika Balkan zilikuwa za kawaida na, kama inavyoitwa na wasomi wa kidini, 'tarjuma zenye muelekeo wa tafsiri', ambapo wasiwasi pekee wa mfasiri ulikuwa kufikisha maana na dhana za aya na hawakuzingatia sana masuala ya  ubora wa lugha au fasihi ya lugha husika.

Uangalifu wa vipengele vya ubora wa lugha ulianza tu katika miaka ya hivi karibuni, kuanzia kwa Esad Durakovic ambaye alikuwa mtaalamu wa elimu na amekuwa akifanya kazi katika uga wa tarjuma na fasihi ya Kiarabu nchini Bosnia Herzegovina kwa miaka mingi.

Mnamo 2004, alichapisha "Qur'ani Tukufu yenye Tarjuma ya Kibosnia", ambayo ni tarjuma nzuri ya Qur'ani Tukufu. Alitumia miaka mingi katika kutayarisha tarjuma ya Qur'ani Tukufu na lengo lake lilikuwa ni kumsaidia msomaji kufurahia kusoma tafsiri ya Quran katika lugha yake ya asili.

Kosovar Faqih na mwanadiplomasia Fatmir Osmania pia walizingatia ubora wa fasihi katika tarjuma zao. Osmani ambaye alikuwa amefanya kazi kwa miaka kumi katika ubalozi wa Kosovo huko London, alijifunza kuhusu kazi za Muhammad Marmaduke Pickthall, mmoja wa watarjumi  wa kwanza wa Qur'ani Tukufu kwa Kiingereza, na akaamua kutarjumi katika Kialbania tarjuma hiyo ya Pickthall ambayo ilikuwa imeidhinishwa na Al-Azhar. Ilikuwa tarjuma ya 12 ya Qur'ani Tukufu katika Kialbania na inajumuisha mtiririko bora kwa mujibu wa fasihi ya Kialbania.

Osmani anasema lengo lilikuwa ni kuandika tarjuma ya Qur'ani Tukufu kwa kutumia viunganishi vichache ili iwe na mtiririko rahisi wa kusoma na kukumbuka.

Wakati wanazuoni wengi wa Kiislamu waliikubali na wakaitisha sherehe ya kuzindua tarjuma hiyo, baadhi yao waliipinga wakisema hakujawa na haja ya kutayarisha tarjuma ya Qur'ani Tukufu kutoka Kiingereza badala ya kutoka Kiarabu ambayo ni lugha asili ya Qur'ani Tukufu.

Mmoja wa wanazuoni walioidhinisha tarjuma ya Osmani ni Shamsi Ivazi, mwanazuoni mashuhuri wa sayansi ya Kiislamu na Kiarabu na mtarjumi wa kazi kutoka Kiarabu hadi Kialbania ambaye anaamini kwamba tarjuma na tafsiri za awali za Qur'ani katika Kialbania zilizingatia tu maana lakini Fatmir Osmani ametegemea tarjuma iliyoidhinishwa na Al-Azhar na kujaribu kufanya jitihada za kutoa tarjuma ambayo inamfanya msomaji wa Kialbania ahisi kuwa anasoma maandishi ambayo yamenufaika na urithi wa fasihi wa nchi yake.

3481729

captcha