IQNA

Wanazuoni Mashuhuri wa Ulimwengu wa Kiislamu /16

Abd al-Razzaq Nawfal; Mwanachuoni aliyeanzisha wazo la Muujiza wa Kisayansi wa Qur'ani Tukufu

19:53 - January 08, 2023
Habari ID: 3476372
TEHRAN (IQNA) – Mwanachuoni na mtafiti wa Kimisri Abd al-Razzaq Nawfal alisoma sayansi ya kilimo lakini akavutiwa na fani ya masomo ya Kiislamu na hivyo akaamua kusoma taaluma ya miujiza ya kisayansi ya Qur'ani Tukufu.

Alikuwa mwanachuoni wa kwanza aliyeanzisha wazo na mijadala kuhusu miujiza ya kisayansi ya Qur'ani Tukufu.

Mnamo 1935, alizungumza juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu na mmoja wa wafanyikazi wenzake ambaye hakuamini kuwa kuna Mungu. Baadaye, alifanya utafiti juu ya suala hilo kati ya 1935 na 1957 na kisha akachapisha kitabu chake cha kwanza  Qur'ani  na Sayansi ya Hadith.

Baadaye, kitabu chake cha pili kilichoitwa "Muujiza wa Nambari katika Qur'ani" kilitolewa.

Katika kitabu hiki, Nawfal hakutaja masomo mengi kuhusu miujiza ya kisayansi ya Qur'ani Tukufu lakini anajulikana kama mtu wa kwanza aliyeibua wazo hilo.

Abd al-Razzaq Nawfal alizaliwa Februari 1917 huko Damietta, Misri. Alipata Shahada ya Kwanza katika sayansi ya kilimo mwaka wa 1938. Kisha akapendezwa na elimu ya dini tukufu ya Kiislamu na  akaandika vitabu juu ya somo hilo. Aliaga dunia mnamo Mei 12, 1984.

Aliandika idadi kubwa ya makala na vitabu kuhusu miujiza ya Qur'ani Tukufu. Kati ya vitabu hivyo ni: "Mungu na Sayansi Mpya", "Muujiza wa Nambari katika Qur'ani Tukufu", "Vilivyoumbwa na Mwenyezi Mungu ", "Muujiza wa Qur'anl", "Ewe Mungu!", "Qur'ani Inaponya", "Waislamu na Sayansi ya Kisasa", na "Qur'ani na Jamii ya Kisasa".

 

captcha