IQNA

Qur'ani Tukufu Inasemaje / 44

Mwenyezi Mungu anaapa kwa tini na zeituni

18:22 - January 16, 2023
Habari ID: 3476410
TEHRAN (IQNA) – Kuna matukio ya kiapo yaliyotajwa ndani ya Qur'ani Tukufu. Mungu Mwenyezi hutumia njia hii anapotaka kuwaambia wanadamu jambo muhimu.

Neno "tini",  limetajwa mara moja katika Qur'an Tukufu na hilo lipo kwenye Surah At-Tin. " Naapa kwa tini na zaituni, Na kwa Mlima wa Sinai! Na kwa mji huu wenye amani!." (aya za 1-3)

Kuna maoni tofauti juu ya kile kinachomaanishwa na "tini na zeituni" hapa. Wafasiri wana mitazamo miwili kwa aya za mwanzo za surah.

Kwanza, inasemekana kwamba kungekuwa na uhusiano kati ya vipengele viwili vya tini na zeituni na viwili vilivyofuata (Mlima Sinai na mji uliosalama). Hivyo, wanasema mtini na mizeituni hurejelea maeneo maalum.

Mlima Sinai ndipo Hadhrat Musa (AS) alipoanza kuzungumza na Mwenyezi Mungu baada ya kurudi kutoka Misri na ndipo alipoteuliwa kuwa nabii.

Baada ya kumaliza ujenzi wa Al-Kaaba, Hadhrat Ibrahim (AS) alisema: “Mola wangu, ifanye ardhi hii iwe salama.” (Surah Ibrahim, aya ya 35)

Kwa hiyo, maneno hayo mawili yanahusu maeneo ya kaskazini mwa Saudi Arabia na Palestina ya leo. Maeneo haya yamekuwa mahali pa kuzaliwa kwa manabii wengi wa Mwenyezi Mungu.

Mtazamo wa pili ni kwamba maneno haya mawili kwa kweli yanarejelea majina ya matunda. Ikiwa ndivyo, basi tunapaswa kuyahusisha vipi na maneno mawili yanayofuata?

Kundi la wafasiri huamini kwamba maneno mawili ya kwanza ni chakula cha mwili na mawili yanayofuata, yanahusiana na roho.

Kwa hiyo, mtu anaweza kuwa na mtazamo mzuri zaidi wa aya inayofuata isemayo: “ Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa. (Surah At-Tin, aya ya 4)

Kwa hiyo, wanadamu wameumbwa kwa namna bora ya kiroho na yenye mlingano.

captcha