IQNA

Wanawake Afghanistan

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wakutana na serikali ya Taliban kuhusu haki za wanawake

17:33 - January 21, 2023
Habari ID: 3476442
TEHRAN (IQNA) - Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina Mohammed, na viongozi waandamizi wa Taliban nchini Afghanistan walifanya mazungumzo kuhusu haki za wanawake.

Mwanadiplomasia huyo mkuu mwanamke wa Umoja wa Mataifa akiwa ameandamana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na masuala ya Wanawake UN Women, Sima Bahous, na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Idara ya Siasa, Masuala ya Kujenga Amani na Operesheni za Amani, Khaled Khiari, wamekamilisha ziara ya siku nne nchini Afghanistan.

Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq aliwaambia waandishi wa habari kwamba ziara hiyo inalenga kutathmini hali, kushirikisha watawala wa sasa wa Afghanistan na kusisitiza mshikamano wa Umoja wa Mataifa na watu wa Afghanistan.

"Katika mikutano na viongozi wa serikali huko Kabul na Kandahar, wajumbe waliwasilisha indahri ya moja kwa moja juu ya amri ya hivi karibuni ya kupiga marufuku wanawake kufanya kazi kwa mashirika ya kitaifa na kimataifa yasiyo ya kiserikali, hatua ambayo inadhoofisha kazi ya mashirika mengi kusaidia mamilioni ya Waafghani walio hatarini ," alisema Haq.

Utawala wa Taliban hivi majuzi ulitangaza kufunga vyuo vikuu vya wanafunzi wa kike nchini kote hadi ilani nyingine, na wamewazuia wasichana kuhudhuria shule za sekondari, kuwanyima wanawake na wasichana uhuru wa kutembea, kuwatenga wanawake katika maeneo mengi ya wafanyikazi na kupiga marufuku wanawake kuingia katika mabustani na kumbi za michezo.

"Ujumbe wangu ulikuwa wazi sana: wakati tunatambua misamaha muhimu iliyotolewa, vikwazo hivi vinawapa wanawake na wasichana wa Afghanistan mustakabali unaowafungia majumbani mwao, kukiuka haki zao na kunyima jamii huduma zao," Mohammed alisema katika taarifa yake. .

"Matarajio yetu ya pamoja ni kwa Afghanistan yenye ustawi ambayo iko kwa amani na yenyewe na majirani zake, na kwenye njia ya maendeleo endelevu. Lakini hivi sasa, Afghanistan inajitenga yenyewe, katikati ya mgogoro mbaya wa kibinadamu na pia ni moja ya mataifa duniani ambayo yanakabiliwa na mabadiliko mabaya ya hali ya hewa."

Kurejea kwa Taliban madarakani nchini Afghanistan mnamo Agosti 15, 2021 na kufuatiwa na kukatizwa kwa usaidizi wa kifedha wa kimataifa kumeiacha nchi hiyo iliyochakaa katika migogoro ya kiuchumi, kibinadamu na haki za binadamu.

Wanawake na wasichana wamenyimwa haki zao, ikiwa ni pamoja na haki ya elimu, na kutoweka kutoka kwa maisha ya umma chini ya Taliban.

Maelfu ya wanawake tangu wakati huo wamepoteza kazi zao au kulazimishwa kujiuzulu kutoka kwa taasisi za serikali na sekta ya kibinafsi.

Wasichana wamezuiwa kuhudhuria shule za kati na upili. Wanawake wengi wametaka haki zao zirejeshwe kwa kuingia mitaani, kuandamana na kuandaa kampeni.

3482150

captcha