IQNA

Mashindano ya Qur'ani Tukufu

Washindi wa Mashindano ya Qur'ani ya UAE watunukiwa zawadi

21:25 - January 24, 2023
Habari ID: 3476455
TEHRAN (IQNA) - Washindi wa toleo la 23 la Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Sheikha Hind Bint Maktoum la Falme za Kiarabu katika kitengo cha wanaume wametunikiwa zawadi.

Sherehe ya utoaji zawadi ilifanyika Dubai siku ya Jumatatu ambapo wale walioshinda mataji ya juu katika kitengo cha wamepokea tuzo zao katika hafla tofauti baada ya sala ya Maghrib siku ya Jumanne.

Kwa mujibu wa Ibrahim Muhammad Bu Melha, mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai (DIHQA), mashindano hayo yalifanyika Januari 7-12.

Ukumbi wa DIHQA katika wilaya ya Al Mamzar ya Dubai uliandaa shindano la wanaume huku wanawake wakishindana katika Jumuiya ya Ufufuo wa Wanawake jijini, alisema.

Bu Melha alibainisha kuwa washindani walishindana katika kategoria za kuhifadhi Qur’ani nzima, kuhifadhi Juzuu 20 , kuhifadhi Juzuu 10, kuhifadhi Juzuu tano (kwa raia wa Imarati), kuhifadhi Juzuu tano (kwa wale walio na zaidi ya miaka 10, na kuhifadhi Juzuu tatu kwa raia wenye umri wa  zaidi ya miaka 10.

Amesisitiza umuhimu kwa kujitokeza watu wengi katika sherehe za utoaji tuzo ili kuwatia moyo washiriki kuendelea katika njia ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu

Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Sheikha Hind Bint Maktoum ni moja ya hafla kuu za Qur'ani zinazoandaliwa na DIHQA kila mwaka.

Mashindano hayo yanalengwa kuwahimiza raia na wahamiaji nchini UAE kujifunza, kuhifadi na kusoma Qur’ani Tukufu sambamba na kutekeleza  mafundisho yake.

 4116691

captcha