IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Usajili wa Mashindano ya Qur'ani ya UAE waanza

15:28 - January 28, 2023
Habari ID: 3476477
TEHRAN (IQNA) – Idara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ilitangaza uzinduzi wa usajili kwa ajili ya mashindano ya 13 ya Qur'ani Tukufu nchini humo.

Ilisema katika taarifa kwamba wale wanaopenda wanaweza kujiandikisha kwa tuzo ya kitaifa ya Qur'ani ya 2023.

Tarehe ya mwisho ya usajili ni Februari 16, idara hiyo ilisema, na kuongeza kuwa duru ya mwisho ya shindano hilo itafanyika kutoka Aprili 24 hadi Mei 12.

Washindani watashindana katika kategoria 9, ikijumuisha kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu kikamilifu, na kuhifadhi na kusoma Juzuu 20.

Kutakuwa na makundi matano ya washiriki kama vile wanafunzi wa shule, wanachama wa taasisi za Qur'ani ambazo hazihusiani na idara hiyo, na wanachama wa vituo vya Qur'ani vinavyohusishwa na idara hiyo.

Washindi watapata zawadi za pesa taslimu kuanzia dirham 5,000 hadi 50,000 za UAE, kulingana na Idara ya Awqaf na Masuala ya Kiislamu.

Mapema wiki hii, washindi wa toleo la 23 la mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Sheikha Hind Bint Maktoum ya nchi hiyo ya Kiarabu walitunukiwa tuzo.

 4117699

captcha