IQNA

Maonyesho ya Qur'ani Tukufu

Nakala 30,000 za Qur’ani zimesambazwa miongoni katika Maonesho ya Vitabu ya Cairo

20:44 - February 02, 2023
Habari ID: 3476504
TEHRAN (IQNA) - Banda la Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia lilikabidhi nakala 30,000 za Qur'ani Tukufu miongoni mwa wageni katika Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Cairo.

Banda hilo lilitoa zawadi ya nakala hizo katika toleo la 54 la maonyesho hayo yaliyoanza nchini Misri Januari 24.

Misahafu hiyo imechapishwa katika Kituo cha Uchapishaji Qur’ani Tukufu cha Mfalme Fahd katika mji mtakatifu wa Madina nchini Saudia.

Kituo hicho huchapisha takriban nakala milioni 10 za Qur’ani Tukufu kila mwaka. Aidha Kituo cha Uchapishaji Qur’ani Tukufu cha Mfalme Fahd kimechapisha tarjuma 55 tofauti za Qur’ani katika lugha karibu 40.

Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Cairo ni maonyesho makubwa na kongwe zaidi ya vitabu katika ulimwengu wa Kiarabu, yanayofanyika kila mwaka katika wiki ya mwisho ya Januari huko Cairo, Misri na huchukuliwa kuwa tukio muhimu zaidi katika ulimwengu wa uchapishaji katika nchi za  Kiarabu. Toleo hili la maonyesho ya vitabu litaendelea hadi Jumatatu, Februari 6.

 4119104

Kishikizo: qurani tukufu ، misri ، saudi arabia
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha