IQNA

Wasomaji bingwa wa Qur'ani Tukufu

Usomaji wa Qur'ani Tukufu wa Sheikh Shuaisha unatoka ndani ya nafsi yake

22:04 - September 26, 2023
Habari ID: 3477657
CAIRO (IQNA) – Visomo vya Qur’ani vya msomaji maarufu wa Misri Sheikh Sheikh Abul Ainain Shuaisha vilitoka kwenye kina cha nafsi yake na ndio maana viligusa nyoyo za wasikilizaji.

Hivi ndivyo Ridha Abdul Salam, mkuu wa Redio ya Qur'ani ya Cairo, alivyomuelezea qari huyo mashuhuri katika chapisho kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Alisema usomaji wa Sheikh Shuaisha ulikuwa wa namna ambayo ungewafanya wasikilizaji kuhisi ukuu na uzuri wa aya hizo.

Msomo huyo wa ngazi za juu alitoka kizazi cha kwanza cha shule ya kisomo cha Misri na akawa nembo shule hii sio tu nchini Misri bali duniani kote, aliongeza.

Abdul Salam alirejelea mojawapo ya visomo vya Shuaisha vya Surah Al-Imran na akasema inaifanya iwe nyepesi nafsi ya wasikilizaji kwa ubunifu na kipaji chake.

Akiwa amezaliwa tarehe 22 Agosti 1922, Abulainain Shuaisha alitumia maisha yake katika kujaribu kufufua mitindo halisi ya qiraa au usomaji Qur’ani. Alielezewa kama mtu mashuhuri katika usomaji wa Qur'an na mmiliki wa 'sauti ya chuma'.

Alianza kusoma Qur'an Tukufu katika umri mdogo na mara akaingia kwenye duru za Qur'ani zilizohudhuriwa na wasomaji mashuhuri. Baadhi wamemchukulia kuwa msomaji ambaye itakwa vigumu kupatikana mfano wake katika uwanja wa usomaji wa Qur’ani Tukufu.

Ustadh Shuaisha alikuwa na sauti halisi ambayo ilielezewa kama "sauti ya chuma" kwa sababu ilikuwa na nguvu sana na kama chuma na ilisikika kwa ubora wa juu zaidi.

Wasoomaji wengi hujaribu kuiga mtindo wa qiraa ya Ustadh Shuaisha lakini hakuna anayeweza kufanya hivyo kikamilifu kwa sababu mtindo na sauti yake vilikuwa vya kipekee na vigumu sana kuiga.

Yeye, pamoja na Ustadh Abdul Basit Abdul Samad, alikuwa mwanzilishi mwenza wa Muungano wa Wasomaji Qur'ani wa Misri, na mwaka 1988, akawa rais wa umoja huo.

Ustadh Shuaisha alisafiri katika nchi nyingi kwa ajili ya kusoma Qur’ani na aliheshimiwa kwa usomaji wake mzuri huko Lebanon, Syria, Iraqi, Uturuki na Jordan, miongoni mwa zingine.

Alikuwa ni Qari wa kwanza wa Misri ambaye alisoma Qur’ani Tukufu katika Msikiti wa al-Aqsa katika mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem).

Ustaidh Shuaisha pia alisafiri hadi Iran mara kadhaa na aliwahi kuwa mjumbe wa jopo la majaji katika mashindano kadhaa ya kimataifa ya Qur'ani nchini humo.

Qari huyo mashuhuri alirejea kwa Mola wake Juni 23, 2011, akiwa na umri wa miaka 89 baada ya kuugua kwa muda wa miezi mitatu.

Hii hapa klipu ya qiraa ya Ustadh Shuaisha

4171029        

 

captcha