IQNA

Shughuli za Qur'ani Tukufu

Misikiti 5,000 ya Misri Kuendesha mafunzo ya Qur'ani Tukufu kwa watoto

14:11 - December 07, 2023
Habari ID: 3478002
CAIRO, (IQNA) - Wizara ya Wakfu ya Misri inapanga kuzindua programu za mfunzo ya Qur'ani Tukufu kwa watoto katika misikiti.

Waziri wa Wakfu Misri Sheikh Mohammed Mukhtar Gomaa alisema misikiti 5,000 kote katika nchi hiyo itakuwa mwenyeji wa hafla hizo za mafunzo ya Qur'ani.

Programu hizi zinazopewa jina la "Mlinde Mtoto Wako kwa Qur'ani", zinalenga kufundisha Qur'ani kwa wanafunzi wa shule za msingi na upili

Mafundisho hayo ya Qur'ani yataandaliwa katika likizo kati ya mihula miwili ya mwaka wa shule, aliongeza.

Waziri Gomaa alibainisha aliangazia shughuli nyingine za  Qur'ani katika wizara yake, akisema pia imezindua programu za Khatm Quran (kusoma Qur'ani Tukufu kuanzia mwanzo hadi mwisho) pamoja na mpango wa kusahihisha namna watu wanavyosoma Qur'ani Tukufu.

Mpango huo unaopewa jina la "Sahihisha Usomaji Wako", unafanyika katika misikiti kadhaa mikubwa katika miji tofauti.

Kila siku baada ya sala za Maghrib na Isha, Imamu wa Sala msikitni au mtaalamu wa kusoma Qur'ani husoma aya za Quran, kuanzia Surah Al-Fatiha, Surah ya kwanza ya Kitabu Kitukufu, na washiriki wanakariri naye  aya moja baada ya nyingine. Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100.

Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.

Shughuli za Qur'ani zimeenea sana katika nchi hii ya Kiarabu ambayo ni maarufu kwa wasomaji wake mahiri wa Qur'ani Tukufu.

 

4186241

Habari zinazohusiana
captcha