IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya 31 ya Qur'ani ya Misri yamepangwa kufanyika Desemba 7-10

20:34 - December 03, 2024
Habari ID: 3479848
IQNA - Mashindano ya 31 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Misri yatang'oa nanga katika mji mkuu Cairo wikendi hii.

Mashindano hayo yamepangwa kufanyika Desemba 7-10, na yatawaleta pamoja wahifadhi wa Qur'ani na wanaharakati kutoka nchi 60, kulingana na Osama al-Jundi, afisa wa Wizara ya Wakfu

Akizungumza katika mahojiano ya televisheni siku ya Jumapili, alisema kuwa kufuatia tathmini za mtandaoni, jumla ya washiriki 141 wameonekana kuwa wamehitimu kushiriki katika mashindano hayo kufikia sasa.

Aliendelea kusema kuwa jumla ya fedha za zawadi zitakazotolewa kwa walioshinda shindano hilo zimefikia pauni milioni 11 za Misri.

Kategoria mpya, yaani tafsiri ya Qur'ani, imeongezwa kwenye tukio la kimataifa katika toleo hili, alibainisha.

Al-Jundi pia alisema kuwa kuandaa mashindano hayo kunaonyesha juhudi za Wizara ya Wakfu ya Misri kukuza Qur'ani Tukufu na kuimarisha hadhi ya Qur'ani katika nchi hiyo.

Toleo la 30 la mashindano ya kimataifa ya Qur'ani lilifanyika Aprili 2024 na wahifadhi kutoka nchi 64 walihudhuria.

Walishindana katika kategoria sita, ikiwa ni pamoja na kuhifadhi Qur'ani nzima pamoja na qiraa na Tafsir, kuhifadhi Qur'ani kwa wasiozungumza Kiarabu, na kuhifadhi Qur'ani kwa maimamu na wahubiri.

3490910

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu misri
captcha