IQNA

Harakati za Qur'ani

Ripoti: Idhaa ya Qur'an ya Misri ina wasikilizaji milioni 60 kila siku

21:43 - June 02, 2024
Habari ID: 3478919
IQNA - Idhaa ya Qur'an ndiyo redio maarufu zaidi nchini Misri, kulingana na mkuu wa redio hiyo.

Mohamed Noor alikuwa akizungumza katika kipindi cha kuadhimisha miaka 90 tangu kuanzishwa kwa Idhaa (Redia)  ya Qur'ani ya MIsri

Alisema takriban watu milioni 60 husikiliza Idhaa ya Qur'ani kila siku, tovuti ya Youm7 iliripoti.

Ameashiria mipango ya hivi majuzi iliyotekelezwa katika Idhaa ya Qur'ani ya kuboresha bidhaa zake na kusema ni pamoja na mipango ya kuendeleza miundo mbinu ya kiufundi, kubadilisha vipindi na kuwaingiza wasomaji wachanga wa Qur'ani.

Mohamed Noor amebainisha kuwa, kwa mara ya kwanza tangu kuzinduliwa kwa Idhaa ya Qur'ani, maqari vijana 12 wamejiunga na idhaa hiyo kama wasomaji Qur'ani.

Idhaa  ya Qur'ani Misri ilianzishwa kwa lengo la kuelimisha na kuzuia upotoshaji wa Qur'ani  na pia kuwasilisha qiraa sahihi ya Qur'ani ya maqari mashuhuri nchini humo.

Tangu kuanzishwa kwake, Idhaa ya Qur'ani imekuwa maarufu sana kwa watu wa Misri na pia nchi zingine ulimwenguni. Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100. Waislamu ni karibu asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo. Shughuli za Qur'ani Tukufu zimeenea sana sana katika nchi za Kiarabu ambapo maqarii wengi maarufu duniani ni Wamisri.

3488590

Habari zinazohusiana
captcha