
Meja Jenerali Mohammad Hossein Baqeri aliyasema hayo Jumatano alipokuwa akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa kongamano la kimataifa la “Jiometri ya Nidhamu Mpya wa Dunia” mjini Tehran.
"Mabadiliko yamekuwa kanuni inayotawala utaratibu wa ulimwengu mzima katika zama tofauti za kihistoria, na kuendelea kwa mfumo Fulani hakumaanishi usahihi wake," alisema, akiongeza kuwa kambi za Mashariki na Magharibi zimetafuta tangu mwanzoni mwa karne ya 20 zilitaka kujifaidhisha, kutawala eneo la Asia Magharibi na kutumia uwezo wake wa kimkakati."
Zaidi ya hayo, Jenerali Baqeri alisema Vita Baridi vilivyodumu kwa muda wa miaka 40 , kutengwa kwa ukomunisti katika milinganyo ya kimataifa, uvamizi wa kikatili wa Marekani dhidi ya Afghanistan na Iraq, na kuundwa kwa kundi la kigaidi la Daesh kwa nia ya kupindua serikali za Iraq na Syria zote zinaashiria ukweli kwamba utaratibu wa dunia unabadilika.”
Alisema zaidi kwamba kuna "ishara kwamba utaratibu wa ulimwengu wote haujapata utulivu" na ulimwengu unakaribia kuingia katika zama ya utaratibu mpya.
Baqeri pia aliutaja uanzishwaji wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni mojawapo ya vikwazo vikuu vya utawala na satwa ya Marekani duniani, akisema kwamba ahadi za Mwenyezi Mungu pia zinaashiria kuanguka kwa mifumo ya kiistikbari na kuanzishwa kwa watu wema badala yake.
Amesisitiza kuwa, utawala ghasibu wa Israel ambao wakati mmoja ulikuwa ukitazama udhibiti wa maeneo ya Waislamu kutoka Mto Nile hadi Euphrates, unazidi kuporomoka na kukumbwa na misukosuko mingi tangu kushindwa kwa fedheha katika hujuma ya siku 33 dhidi ya Lebanon katika majira ya joto ya mwaka 2006.
"Taifa linalodhulumiwa la Palestina na Mhimili wa Muqawama, kwa upande mwingine uko kwenye kilele cha mamlaka yao, na wanasonga mbele kwenye njia ya ukombozi wa Palestina," Baqeri alibainisha.
Afisa huyo wa ngazi za juu wa jeshi la Iran aidha alibainisha kuwa, China imeichukua Marekani kama nchi yenye uchumi mkubwa zaidi duniani, na nia yake ya kuwekeza katika bara la Asia na baadhi ya maeneo ya Afrika na Ulaya inaonyesha wazi kwamba jiometri mpya ya utaratibu wa dunia imeanza kujitokeza.
4139953