IQNA

Diplomasia

Akiwa Uganda, Rais wa Iran awashambulia Wamagharibi kwa kutetea vitendo vichafu

15:39 - July 13, 2023
Habari ID: 3477275
KAMPALA (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyashambulia madola ya Maagharibi kutokana na hatua yao ya kutetea vitendo vichafu vya ushoga na mahusiano ya kingono ya watu wa jinsia moja.

Rais Rais Ebrahim Raisi alisema hayo kabla ya kukamilisha safari yake nchini Uganda na kuelekea Zimbabwe leo  ambapo alisisitiza kwamba, madola ya Magharibi yamekuwa yakihujumu misingi ya familia kutokana na kupigia debe uchafu wa mahusiano ya kingono ya watu wa jinsia moja.

Rais wa Iran amekosa vikali tabia ya madola ya Magharibi ya kutumia suala la haki za binadamu kwa ajili ya kushinikiza mataifa huru kama ambavyo ameyakosoa kwa hatua yao ya wa kueneza vitendo vya ushoga, misimamo ya kufurutu ada na ugaidi.

Kadhalika Rais Ibrahim Rais sambamba na kuashiria kwamba, hatua hiyo inalenga kusambaratisha kizazi cha mwanadamu amesifu misimamo ya Uganda kuhusiana na suala hilo.

Ibrahim Rais amepongeza pia misimamo ya Iran na Uganda iliyo dhidi ya misimamo ya kufurtu ada na ugaidi na kueleza kwamba, nukta ya ushirikiano baina ya Kampala na Tehran ni utambulisho wao ulio dhidi ya ukoloni.

Kabla ya kukamilisha safari yake nchini Uganda na kuelekea Zimbabwe, akiwa mjini Kampala, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa dini mbalimbali nchini Uganda akiwemo Mufti Mkuu wa nchi hiyo Shekhe Shaaban Ramadhan Mubaje.

Kauli ya Rais Museveni

 

Katika hotuba yake, Rais Yoweri Museveni amesema: "Siku zote tuko tayari kushirikiana na Iran," na kuongeza kuwa ushirikiano huo unatokana na msimamo wa Iran wa kupinga ubeberu na kusema hiyo ndiyo sababu ambayo imepelekea atembelee Iran.

Rais Museveni alimwambia mwenzake wa Iran na ujumbe wake kwamba hakuna chochote Uganda haiwezi kuzalisha katika sekta ya kilimo kwa sababu ya hali ya hewa nzuri. Alitaja bidhaa hizo ni pamoja chakula; ndizi, mahindi, kahawa, kakao na samaki akiongeza kuwa tatizo daima limekuwa ni upatikanaji wa masoko na ushirikiano wa Iran unakuja kwa manufaa.

"Tunaweza kufanya biashara nyingi pamoja. Iran ina uzoefu ambao hatuna," Rais Museveni aliongeza.

Rais Museveni aliishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kumhamasisha kuendeleza mradi wa uchimbaji mafuta ya petrol nchini Uganda hasa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta nchini Uganda.

"Tuna mafuta kidogo hapa ambayo tuligundua miaka michache iliyopita. Nilikuwa na baadhi ya watu wanaotukatisha tamaa kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta wakisema hakina faida, nilishangaa kwa nini nchi nyingi zinaendelea kuwa na viwanda vya kusafisha mafuta kama havina faida!." Rais Museveni alisema alipotembelea Iran, alifahamishwa kuwa nchi hiyo ya Kiislamu ina viwanda tisa vya kusafisha mafuta na viko katika hatua za juu za kujenga vingine.

"Kwa hivyo, niliporudi, niliweka nilisema tunajenga kiwanda cha kusafisha mafuta na kuendeleza sekta ya petrokemikali. Kwa hivyo, unaweza kuona maeneo ya kukamilishana na ningewasihi mawaziri walichukulie kwa uzito suala hili," Museveni alisema.

Kabla ya kukamilisha safari yake nchini Uganda na kuelekea Zimbabwe, akiwa mjini Kampala, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa dini mbalimbali nchini Uganda akiwemo Mufti Mkuu wa nchi hiyo Shekhe Shaaban Ramadhan Mubaje.

4154767

captcha