IQNA

Ifahamu Qur'ani Tukufu / 27

Kamanda ambaye askari wake hawashindwi

11:11 - August 29, 2023
Habari ID: 3477515
TEHRAN (IQNA) – Kuna kamanda hodari ambaye sio tu kwamba hajawahi kushindwa bali pia hawaweki askari wake katika mazingira ya kushindwa.

Kamanda huyu yuko ulimwenguni kote na huwafunza askari kila wakati. Kamanda huyu ni nani na anawezaje kuwepo duniani kote?

Katika historia, kumekuwa na wapiganaji wengi na mashujaa wa kijeshi ambao walipata heshima kwenye njia ya kufikia malengo yao. Kawaida, mafanikio ya mtu wa kijeshi hupimwa na ushindi wake au kushindwa katika vita kuu na vya maamuzi. Itakuwa ajabu kujua kwamba kuna kamanda ambaye hajawahi kushindwa.

Imam Ali (AS) alisema kuhusu Qur'ani Tukufu katika Khutba ya 198 ya Nahj al-Balagha kwamba: “… Heshima ambayo wafuasi wake hawashindwi, na ukweli ambao wasaidizi wake hawakuachwa.

Sasa swali linaibuka hapa kwa sababu ni wazi kwamba Waislamu (wafuasi na waungaji mkono wa Qur'ani Tukufu) walishindwa katika baadhi ya vita, vikiwemo vita vya Uhud.

Jibu ni kwamba Qur'ani Tukufu haiwaachi wafuasi wake kushindwa maadamu wao (Waislamu) wanatekeleza mafundisho yake. Vinginevyo, itakuwa wazi kwamba watashindwa.

Kwa mfano, kuna aya katika Qur'ani Tukufu inayowaamrisha Waislamu kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Waislamu walishindwa katika Vita vya Uhud kwa sababu waliasi amri hii.

Nukta nyingine ni kwamba kushindwa huku na mfano wao katika dunia hii ni kushindwa kwa wanaadamu kwani ukweli wa Uislamu na Quran haudhuriki na kushindwa huko.

Qur’ani Tukufu inasema: “…Wanasema: Lau ingelikuwa tuna lolote katika jambo hili tusinge uliwa hapa. Sema: Hata mngeli kuwa majumbani mwenu, basi wangeli toka walio andikiwa kufa, wakenda mahali pao pa kuangukia wafe.(Haya ni hivyo) ili Mwenyezi Mungu ayajaribu yaliyomo vifuani mwenu, na asafishe yaliyomo nyoyoni mwenu. Na Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo vifuani.” (Aya ya 154 ya Surah Al-Imran)

Kwa hivyo, ikiwa Waislamu daima watafuata mafundisho ya Qur'ani Tukufu, watakuwa washindi daima. Vinginevyo, watapata kushindwa. Zaidi ya hayo, wakati Fulani Mwenyezi Mungu anataka kuwajaribu Waislamu na hivyo wanashindwa katika mapambano  na ikiwa wataendelea kuwa na subira na kuwa na ustahamilivu, ushindi wa mwisho utakuwa wao.

captcha