IQNA

Ifahamu Qur'ani Tukufu /15

Kitabu kinachosadikisha vitabu vilivyotangulia vya Mwenyezi Mungu

17:18 - July 18, 2023
Habari ID: 3477303
TEHRAN (IQNA) – Katika Qur'ani Tukufu Aya ya 3 ya Sura Al Imran, Mwenyezi Mungu anasema ameteremsha Qur'ani Tukufu ambayo inasadikisha vitabu kabla yake ambavyo ni Taurati na Injili

Je, uthibitisho huu una maana gani kutokana na kwamba Qur'ani imeteremshwa kama kitabu kitakatifu baada vitabu hivyo vlivyotajwa?

 Amekuteremshia Kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili  (ya Nabii Isa au Yesu iliyo potea)."  (Aya ya 3 ya Surah Al Imran)

Hii ni miongoni mwa aya za Qur'ani Tukufu zinazothibitisha kwamba kuna dini moja tu mbele ya Mwenyezi Mungu.

Dini ni moja na huko ni kunyenyekea kwa Mungu. " 9. Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu." (Aya ya 19 ya Surah Al Imran)

Vile vile tunasoma katika Aya ya 85 ya Sura hii (Al Imran): “Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri."

Yale ambayo yamekuja katika mfumo wa Uislamu, Ukristo, Uyahudi, n.k, ni tamaduni tofauti za kidini ambazo zote zinalazimu kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu. Asili ya kweli ya mapokeo haya ya kidini ni moja na bila kupingana au kutofautiana. Kwa mujibu wa Quran, tofauti zinazoonekana katika vitabu vya Mwenyezi Mungu vilivyotufikia ni kwa sababu ya mabadiliko yaliyofanywa ndani yake na baadhi ya watu. " Na wapo baadhi yao wanao pindua ndimi zao katika kusoma Kitabu ili mdhanie kuwa hayo yanatoka Kitabuni, na wala hayatoki Kitabuni. Na husema: Haya yametoka kwa Mwenyezi Mungu. Na wala hayatoki kwa Mwenyezi Mungu. Na wanamsingizia Mwenyezi Mungu uwongo na wao wanajua." Aya ya 78 ya Surah Al Imran.

Nukta nyingine ni kwamba tofauti za mila za kidini zinatokana na ukamilifu zaidi katika baadhi. Hebu fikiria unampa kijana vitabu vitatu na kumwambia cha kwanza kitasaidia ujuzi wake kukua kwa 20%, cha pili kitasaidia ujuzi wake kukua kwa 45% na cha tatu kitasaidia ujuzi wake kukua kwa asilimia 90.

Vitabu hivyo vitatu havipingani bali kila kimoja kina uwezo tofauti wa kumsaidia mtu kukua.

Mwenyezi Mungu, katika Aya ya 3 ya Surah Al Imran, anasema Qur'ani Tukufu imeteremshwa kwa Haq (haki). Haq asili yake inamaanisha maelewano na mlingano.

Kuiteremsha Qur'ani Tukufu pamoja na Haq maana yake ni jambo lisilopingika na kwamba hakuna uwongo ndani yake.

captcha