Qur'ani Tukufu ni kitabu kitukufu cha Waislamu ambacho kiliteremshwa kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) katika kipindi cha miaka 23. Msingi wa Qur'ani Tukufu ni matakwa ya Mwenyezi Mungu na hakuna yeyote, hata Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) amekuwa na haki ya kuibadilisha yaliyomo.
Tunasoma katika Aya ya 44-46 ya Sura Al-Haqqa: “Na lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu, bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia. Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo!"
Baadhi ya aya za Qur'ani Tukufu zina sifa maalum zinazoashiria kwamba Mwenyezi Mungu, Mwenyewe, ndiye anayezisema bila shaka yoyote:
Nini maana ya Nuzul (kuteremsha) ya Qur'anI Tukufu ? Tunapozungumzia Nuzul, maana yake kuna sehemu ya juu ambayo kitu kinashuka. Qur'anI Tukufu imeteremshwa kutoka ulimwengu wa juu hadi kwenye ulimwengu huu lakini haimaanishi kuwa Mwenyezi Mungu ana nafasi mbinguni na ameiteremsha Qur'ani Tukufu kutoka mahali hapo bali inaonyesha hadhi ya juu ya Mwenyezi Mungu (Mwenyezi Mungu yuko kila mahali).