IQNA

Ifahamu Qur'ani Tukufu /38

Kitabu ambacho msomaji wake anapaswa kufuata taratibu maalum

19:30 - November 12, 2023
Habari ID: 3477883
TEHRAN (IQNA) – Kwa kawaida, hakuna utaratibu au nidhamu maalum zinazohitajika kwa ajili ya kusoma kitabu. Lakini kuna kitabu kinapatikana katika nyumba ya kila Mwislamu ambacho usomaji unahitaji utaratibu na nidhamu maalum.

Kitabu hicho ni Qur'ani Tukufu. Na moja ya masuala yanayopewa umuhimu katika kusoma Qur'ani Tukufu ni utaratibu wa usomaji ambao unajulikana kama Tilawah.

Ina maana ya kusoma Qur'ani Tukufu huku ukizingatia mpangilio maalum uliopo baina ya aya pamoja na kutafakari ujumbe mkuu na maana za Aya.

Lengo katika aina hii ya usomaji ni ustawi wa mawazo na maadili ya mwanadamu, ili kuepusha uibukaji wa tabia mbovu.

Hili ni muhimu sana kiasi kwamba Mungu anaamuru Mtume wake kusoma Qur'an wakati wa usiku:

“Ewe uliye jifunika! Kesha usiku kucha, ila kidogo tu!. Nusu yake, au ipunguze kidogo.. Au izidishe - na soma Qur'ani kwa utaratibu na utungo." (Aya ya 1-4 ya Surah Al-Muzzammil)

Wakati mtu anataka kukutana na mtu anayeheshimiwa, huvaa nguo zake bora na manukato. Kwa hakika, kusoma Qur'ani Tukufu, Kitabu Kinachoheshimika  na ambacho ni muhimu sana, kunahitaji uzingatiaji wa adabu ambao unaonyesha jinsi tunavyokiheshimu Kitabu hiki Kitakatifu. Baadhi ya adabu hizo ni pamoja na kutawadha, kuchunga Tahara (kuwa msafi kimwili na kiroho), kupiga mswaki n.k.

Kuzingatia haya kutatusaidia kufaidika zaidi na Qur'ani Tukufu.

Neno Tarteel (lililotumika katika Aya ya 4 ya Surah Al-Muzzammil) linasisitiza haja ya kusoma Qur'ani Tukufu pamoja na kutafakari maudhui na maana ya aya. Ingawa tunafaidika na Qur'ani Tukufu kwa kusoma tu, tutabarikiwa hata zaidi kwa kutafakari dhana za Kitabu Kitukufu.

Imam Sadiq (AS) amesema: “Tarteel maana yake ni kwamba katika kusoma Quran, unapofikia aya zinazohusu pepo, muombe Mwenyezi Mungu akupe pepo na unapozifikia aya zinazohusu moto, kimbilia kwa Mwenyezi Mungu."

Moja ya baraka za kusoma Quran ni kuipa nafsi utulivu , kwani aya za Kitabu hicho kitukufu zinatukumbusha juu ya Mwenyezi Mungu. “Kwa hakika kwa, kumkumbuka Mwenyezi Mungu huleta utulivu kwa mioyo yote.” (Aya ya 28 ya Surah Ar-Ra'ad)

captcha