IQNA

Ifahamu Qur'ani Tukufu / 37

Kitabu Kinachotuambia Kuhusu Zamani, Sasa, na Wakati Ujao

14:52 - November 05, 2023
Habari ID: 3477843
TEHRAN (IQNA) – Watu hushangaa mtu anapotoa utabiri kuhusu siku zijazo, lakini inashangaza zaidi kujua kwamba kuna kitabu ambacho kimetabiri kwa usahihi kuhusu siku zijazo.

Wakati watu wanatabiri, wanafanya kulingana na uchambuzi wao wa hali ya zamani na ya sasa. Wanadhani kwamba kwa mujibu wa uchambuzi huu, hii au ile inaweza kutokea katika siku zijazo.

Vipi kuhusu utabiri wa Qur'ani Tukufu? Kitabu ambacho kimeteremshwa wakati fulani na chini ya hali fulani kinawezaje kutabiri kuhusu mustakabali? Hapa kunaweza kuwa na maelezo mawili ambayo yote ni ya kweli na hayapingani.

  • Mifano ya namna ambavyo Qur'ani Tukufu inazungumza kwa uwazi kuhusu yatakayotokea siku za usoni

Mfano mmoja ni vita kati ya Iran na dola la Kirumi ambapo Qur'ani Tukufu ilitoa utabiri wa wazi ambao ulitimia. Wakati wa utawala wa mfalme wa silsila ya Sasania, Khusrow Parviz, Iran iliwashinda Warumi vikali. Hakuna aliyefikiri kwamba Warumi, ambao walikuwa wameshindwa sana na kudhoofishwa wangeweza kupigana na kuishinda Iran. Lakini Qur'ani Tukufu ilitabiri kwamba ingetokea na ikawa:

“Warumi wameshindwa (na Waajemi) katika ardhi iliyo karibu. Lakini, katika miaka michache baada ya kushindwa kwao watakuwa washindi. Katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi.” (Aya 2-4 za Surah Ar-Rum)

  • Mifano ambayo watu wa kawaida hawawezi kuielewa

Watu wa kawaida hawawezi kufahamu undani wa mafundisho na ukweli wa Qur'ani Tukufu, ambao ni wa hali ya juu sana na hivyo ni Mtume Muhammad (SAW) na watu wa nyumba yake yaani Ahul Bayt (AS) wanoweza kuelewa wanaweza kuelewa.

Mathalan, Imamu Sadiq (AS) alikuwa mjuzi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kile kinachosema kuhusu mwanzo wa uumbaji na chochote kitakachotokea hadi Siku ya Kiyama.

Kwa hivyo kila kitu kimetajwa ndani ya Qur'ani lakini si watu wote wenye uwezo wa kukifahamu.

captcha