IQNA

Ifahamu Qur'ani Tukufu/29

Qur'ani Tukufu: Kitabu ‘Kilichotelekezwa’

21:31 - September 04, 2023
Habari ID: 3477548
TEHRAN (IQNA) – Kuna aya ndani ya Qur’ani Tukufu inayoashiria umuhimu wa kitabu, ikimnukuu Mtukufu Mtume (SAW) kwamba watu wake “wamekiacha” kitabu hicho.

Mojawapo ya aya zenye kuchochea fikira na muhimu zaidi katika Qur'ani Tukufu inahusu aya ya 30 ya Sura Furqan. Katika aya hii, Mwenyezi Mungu anafikisha ujumbe kutoka kwa Mtume kuhusu Siku ya Kiyama: “ Na Mtume alikuwa akisema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wameifanya hii Qur'ani ni kihame."

Hadithi nyingine ya Imam Baqir (AS) inatoa mwanga juu ya kipengele kingine cha suala hilo. Hadith inasema:

Siku hiyo Mola Mtukufu atasema: “Ewe dalili yangu katika Ardhi na sauti ya Mtume wangu mkweli, inua kichwa chako na omba maombi yako, kwani yatapewa, na uombee ili maombi yako yakubaliwe. umewapata watumishi wangu?" Hivyo, Qur'ani Tukufu inasema: "Ewe Mola wangu, baadhi yao walishikilia mafundisho yangu na hawakupoteza chochote, na wengine walinidharau, wakanidhalilisha, na wakanusha ujumbe wangu, licha ya jukumu langu la kuongoza kwa viumbe vyote." Kisha Mungu anasema: “Naapa kwa enzi yangu, leo nitakulipa malipo bora kabisa na nitawaadhibu wale ambao wamekuletea maumivu makali zaidi.

Majadiliano haya yana umuhimu mkubwa, kwani yanatajwa sio tu katika Qur'ani Tukufu bali pia katika mafundisho ya Ahlul-Bayt (AS). Umuhimu wake unaenea zaidi kwa sababu furaha au huzuni ya watu binafsi inategemea kushikamana kwao na Qur'ani Tukufu.

Mullah Mohsen Fayz Kashani, msomo mashuhuri wa madhehebu ya Shia, alielezea uzoefu wake kuhusu kupuuzwa kwa Qur'ani Tukufu na athari zake kwa mwongozo wa mwanadamu. Alisema, "Niliandika vitabu, nilifanya utafiti, lakini sikupata dawa ya maumivu yangu, sikupata maji kwa ajili ya kiu yangu; niliogopa na kumgeukia Mwenyezi Mungu kwa maombi mpaka Qur'ani Tukufu na Hadithi zikaniongoza."

Baadhi ya tafsiri zinafafanua kupuuza kuwa ni kutoisoma Qur'ani Tukufu, kushindwa kuifanya kuwa msingi katika maisha ya mtu, kupuuza kuitafakari, kutoifanyia kazi, na kupuuza kuifundisha wengine. Katika tafsiri nyingine, hata kushindwa kufuata aya moja ni kutoijali Qur'ani Tukufu.

Kwa hiyo, wale wanaotaka kuepuka lawama kutoka kwa Mtume (SAW) na Qur'ani Tukufu Siku ya Kiyama ni lazima wajishughulishe kwa bidii katika kusoma Qur'an na kushikamana na mwongozo wake.

Katika riwaya nyingine, Imam Baqir (AS) amemnukuu Imam Ali (AS) akisema: “Mimi ni ukumbusho ambao watu walipotea, njia waliyoiacha, imani waliyoikufuru, Qur'ani waliyoiacha, na dini waliyoikanusha. ."

Riwaya hii inatusaidia kuelewa kwa nini Imam Ali (AS) alikuwa rejea ya Qur'ani Tukufu.

Alikuwa ni Qur'ani hai ambayo maneno yake yalikusudiwa kufuatwa chini ya hali zote. Hata hivyo, historia inadhihirisha kwamba watu wa zama zake walimdhulumu na nafasi ya haki ya Imam ilichukuliwa kutoka kwake isivyo haki.

Ufahamu wa Qur'ani unapaswa kujikita katika tafsiri za Maimamu (AS). Maelezo haya ya kihistoria yanaonyesha jinsi tafsiri potofu kubwa ilivyosababisha kuachwa kwa maana halisi ya Qur'ani Tukufu.

captcha