IQNA

Ifahamu Qur'ani Tukufu / 32

Bahari ambayo kina chake hauwezi kutasawari

20:45 - October 01, 2023
Habari ID: 3477680
TEHRAN (IQNA) – Wakati watu wanapotaka kuashiri kina cha fikra, maudhui au kitu kingine chochote, wanakifananisha na bahari.

Qur'ani  Tukufu pia inafananishwa na bahari kwa sababu ya kina chaka

Imam Ali (AS) katika Khutba ya 198 ya Nahj al-Balagha, ambayo ni khutba ya kina kuhusu sifa za Qur'ani Tukufu, anasema: “Kisha, Mwenyezi Mungu akampelekea Kitabu kama nuru ambayo miali yake haiwezi kuzimika, taa ambayo mwanga wake haufifii, bahari ambayo kina chake hakiwezi kupimika…”

Neno bahari limetumika kurejelea Qur'ani Tukufu kutokana na sababu kadhaa zikiwemo:

  1. Siri za Qur'ani Tukufu

Quran Tukufu, ambacho ni kitabu cha mwisho cha Kimungu kilichoteremshwa kwa mjumbe wa mwisho wa Mwenyezi Mungu, yaani Mtume Muhammad (SAW), kina siri ambazo zinajulikana na Mwenyezi Mungu pekee na Maasumin 14 (AS). Ndiyo maana mawazo na akili ya watu wengine, bila kujali ni kiasi gani wanaogelea katika bahari hii ya kina, haiwezi kufikia mwisho wake.

Imamu Sadiq (AS) alisema: “Mimi ni mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na nina elimu na utambuzi kuhusu Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Ndani ya Qur'ani Tukufu kuna (elimu ya) yale yanayohusiana na mwanzo wa uumbaji na yatakayokuwa mpaka Siku ya Kiyama. Katika Qur'ani Tukufu kuna habari za mbingu na ardhi, pepo na moto, na zamani na sasa. Ninawajua kama sehemu ya nyuma ya mkono wangu."

Katika Hadith nyingine, Imam Sadiq (AS) anahusisha elimu yoyote aliyonayo na Qur'ani Tukufu, akisema amepata elimu yake kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kwamba maelezo ya kila kitu yamo ndani ya Qur'ani Tukufu.

Kwa hiyo, kwa kuzingatia Hadithi hizi, Maimamu Maasumin (AS) wana elimu ya Qur'an wakati fikira na akili za watu wa kawaida haziwezi kufahamu kikamilifu elimu hiyo kwa kujitegemea.

  1. Ubora wa Qur'ani Tukufu

Kipengele kingine cha kufananisha Qur'ani Tukufu na bahari ni kwamba kama vile bahari ilivyojaa vito na vya kupendeza, Qur'ani Tukufu ndio chimbuko la fadhila na mambo yote mazuri.

Mtukufu Mtume (SAW) alisema kuhusu ubora wa Qur'anI Tukufu : “Ubora wa Neno la Mwenyezi Mungu juu ya maneno mengine ni kama ubora wa Mwenyezi Mungu juu ya viumbe vyake."

3485380

captcha