IQNA

Ifahamu Qur'ani Tukufu / 28

Njia bora zaidi za kumkaribia Mwenyezi Mungu

20:38 - September 02, 2023
Habari ID: 3477536
TEHRAN (IQNA) – Wanadamu daima huwa wanatafuta njia za kufikia matamanio na matakwa yao yote.

Je! ungependa kugundua hazina kama hiyo haraka iwezekanavyo? Endelea kusoma.

Kwa sababu Mwenyezi Mungu ndiye chanzo cha baraka zote duniani, mtu anapaswa kumwomba ili kufikia matamanio yake. Kwa mujibu wa vyanzo vya kidini, njia bora ya kumwomba Mwenyezi Mungu ni kupitia Qur'ani Tukufu.

Kuomba kitu ni njia ya kukidhi mahitaji. Mwenyezi Mungu ndiye pekee anayejua mahitaji yote ya wanadamu na kuyatimiza. Wakati mwingine inaweza kuonekana kuwa mtu mwingine ametimiza hitaji letu lakini ukweli ni kwamba hata mtu huyo ni wakala wa Mwenyezi Mungu kwa kujua au kutojua. Ikiwa Mwenyezi Mungu hataki jambo fulani litokee, halitatokea na tatizo halitatatuliwa hata kama watu wote duniani watajaribu kulitatua.

Imam Ali (AS) anasema katika Khutba ya 176 ya Nahj al-Balagha: “Muombee Mwenyezi Mungu kupitia kwayo na urejee kwa Mwenyezi Mungu kwa mapenzi yake. Usiwaulize watu kupitia hilo. Hakuna kitu kama hicho ambacho kwacho watu watarejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu."

Akifafanua sehemu hii ya khutba, Ayatullah Nasser Makarem Shriazi anaandika: Imam Ali (AS) anatuamuru tumuombe Mungu tunachotaka kupitia Qur'ani Tukufu. Maana yake ni kwamba tunapaswa kujipamba kuwepo kwetu kwa mafundisho na muongozo wa Qur'ani Tukufu na tujitayarishe kwa yale tuliyoomba tupewe. Vile vile tunapaswa kuigeukia Qur'an Tukufu kwa upendo kwa sababu kila anayekipenda Kitabu Kitukufu atatekeleza mafundisho yake na kwa njia hiyo atarejea kwa Mwenyezi Mungu kwa njia ifaayo.

Imam Ali (AS) pia anatutaka tusiulize kupitia Qur'ani Tukufu kutoka kwa watu wengine. Hii inaonyesha kuwa baadhi ya watu wanaitumia Qur'ani Tukufu kufikia malengo yao ya kidunia.

Imam Sadiq (AS) amesema katika Hadith kwamba maqari wa Qur'ani Tukufu ni makundi matatu: Wale wanaosoma Qur'ani ili wengine wawasifu, na wale wanaosoma Qur'ani ili wapate manufaa ya kidunia. Hakuna kheri katika kusoma Qur'ani kwa madhumuni haya. Lakini kuna kundi la watu wanaosoma Qur'ani katika sala zao mchana na usiku ili kunufaika kiroho.

Imam (AS) anatuonya tusiwe miongoni mwa makundi mawili ya mwanzo na anatuhimiza kutumia Qur'ani Tukufu kama njia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa hiyo kila mtu anapaswa kuweka kipaumbele chake cha kwanza kumjua Mwenyezi Mungu zaidi kupitia Qur'ani na kumkaribia zaidi. Ikiwa mtu ana makusudio mengine anapokiendea Kitabu Kitukufu, atakuwa katika hasara kubwa.

captcha