IQNA

Jiografia ya Matukio katika Qur'ani Tukufu /1

Firdaus walimokuwa Adam na Hawa ilikuwa Wapi?

10:18 - November 09, 2023
Habari ID: 3477863
TEHRAN (IQNA) – Adam (AS) alikuwa mtume wa kwanza aliyeishi Jannat Firdaus (Peponi au Paradiso) baada ya kuumbwa na Mwenyezi Mungu.

Adam (AS) alipomuasi  Mwenyezi Mungu, alifukuzwa Jannat Firdaus na kupelekwa duniani.

Swali ambalo baadhi ya wasomi na watafiti wamejaribu kujibu ni kwamba paradiso au peponi alimokuwemo Nabii Adam (AS) hii ilikuwa na sifa gani.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 35 ya Sura Al-Baqarah: “Tukamwambia Adam: “Na tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani (peponi), na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu tu; mkawa katika wale walio dhulumu..”

Kuna mitazamo tofauti miongoni mwa wanachuoni na wafasiri wa Qur'an Tukufu kuhusu Jannat Firdaus ambayo Adam (AS) na Hawa walikuwa wakiishi. Wengine wanasema ni Jannat Firdaus ile ile ya milele ambayo watu wema wataingia na kuishi akhera huku wengine wakisema kwamba eneo hilo ilikuwa duniani.

Sababu ambayo kundi la mwisho linaitaja ni kwamba Shetani hataweza kufika Jannat Firdaus ya milele lakini aliingia peponi ambapo Adam (AS) na Hawa waliishi na kisha akawahadaa:

  “Lakini Shet'ani alimtia wasiwasi, akamwambia: Ewe Adam! Nikujuulishe mti wa kuishi milele na ufalme usio koma?’” (Aya ya 120 ya Surah Taha).

Zaidi ya hayo, kuingia katika Jannat Firdaus ya milele kunamaanisha kukaa humo milele. Kwa mujibu wa Hadith, Imamu Sadiq (AS) alisema kwamba Firdaus ya Adam (AS) ni miongoni mwa bustani za dunia ambazo jua na mwezi ziliangaza juu yake na lau ingelikuwa ni pepo ya milele, asingefukuzwa humo.

Sasa swali ni kwamba Jannat Firdaus ya Adamu (AS) ilikuwa wapi duniani.

Kwa mujibu wa Torati, kulikuwa na mto katika paradiso hiyo ambao uligawanywa katika vijito vinne vya Pishoni, Gihoni, Hidekeli (Tigris), na Frati (Euphrates).

Lakini bila kujali maoni ya Torati kuhusu mito hii, kuna maoni mbalimbali juu ya mahali pepo ya Adamu ilikuwa:

1- Wengine wanasema pengine ilikuwa katika Quds tukufu. Wanarejea Aya ya 58 ya Sura Al-Baqarah isemayo: “(Enyi Wana wa Israili, kumbukeni neema Zangu) Na tulipo sema: Ingieni mji huu, na humo mle mpendapo maridhawa, na ingieni katika mlango wake kwa unyenyekevu, na semeni: Tusamehe! Tutakusameheni makosa yenu, na tutawazidishia wema wafanyao wema.”

Al-Quds (Jerusalem) ni moja ya miji mikongwe zaidi ulimwenguni na mahali patakatifu katika Uislamu, Ukristo na Uyahudi.

2- Baadhi ya wengine wanasema pepo ambayo Adam (AS) na Hawa walikaa ilikuwa ni Firdaus ya Aden iliyokuwa Mesopotamia, katika Iraq ya leo.

Mesopotamia ni eneo la kihistoria la Asia Magharibi ambalo liko ndani ya mfumo wa mto Tigris-Euphrates, katika sehemu ya kaskazini ya Hilali yenye Rutuba ( Chimbuko la Ustaarabu) Kwa maana pana, eneo hilo pana la kihistoria lilijumuisha Iraq ya sasa na sehemu za Iran ya sasa, Kuwait, Syria na Uturuki.

Kishikizo: qurani tukufu adam hawa
captcha