IQNA

Shakhsia katika Qur’ani/1

Adam (AS), mwanadamu wa kwanza au Nabii wa kwanza?

23:48 - July 23, 2022
1
Habari ID: 3475530
TEHRAN (IQNA)- Adamu (AS) ndiye baba wa jamii ya sasa ya mwanadamu na halikadhalika alikuwa Nabii kwa kwanza. Mwanadamu wa kwanza ndiye aliyekuwa Nabii wa kwanza ili mwanadami asiachwe kamwe bila mwongozo.

Nabii Adam (AS), kulingana na imani ya Uislamu, Uyahudi na Ukristo, ni baba wa wanadamu wote wanaoishi leo. Kulingana na Hadiths za Kiisilamu, Adam (AS) sio mwanadamu  wa kwanza kuishi duniani kwani kulikuwa na wanadamu wengine ambao kizazo chao kiliangamia kabla yake..

Wanadamu wa leo ambao ni kizazi cha Adam (AS) na hawana uhusiano na wanadamu ambao waliishi kabla yake.

Qur’ani Tukufu inamuelezea Adam (AS) kama aliyechaguliwa:  “Hakika Mwenyezi Mungu alimteuwa Adam na Nuhu na ukoo wa Ibrahim na ukoo wa Imran juu ya walimwengu wote.” (Qur’ani Tukufu, Sura Aal Imran aya ya 33)

Hii ndio sababu wakati Waislamu wanataka kuzungumza kuhusu mwanzo na mwisho wa Utume husema ‘ kutoka Adam hadi Khatam (Mtume wa Mwisho).

Ukweli kwamba Adamu (AS) alichaguliwa kama Nabii ni ishara  kwamba Mwenyezi Mungu hajawahi kumuacha mwandamu bila mwongozo.

Jina Adam limetajwa mara 25 katika Surah 9 za Qur’ani Tukufu. Katika hadithi za Kiisilamu, Adam (AS) ametajwa kama Abul Bashar (baba wa ubinadamu), Khalifatullah (naibu wa Mwenyezi Mungu au Makamu), na Safiullah (aliyechaguliwa na mwenyezi Mungu).

Katika aya kadhaa, kama vile aya 5 wa Surah al-Hajj, aya ya 71 wa Surah Saad, aya ya 11 wa Surah As-Saaffat, aya ya 48 wa Sura al-Hijr, aya ya 14 wa Surah al-Rahman, na aya ya 7 ya Surah As-Sajdah, Qur’ani inataja kuhusu uumbaji wa Adam kutoka kwa vumbi na udongo. Katika aya ya 12 ya Surah al-Muminun Mwenyezi Mungu anasema: " Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo." Na katika aya ya 26 ya Surah al-Hijr tunasoma: " Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura."

Aya hizi zinaelezea awamu za uundaji wa mwili wa Adam kutoka kwa vumbi hadi mchanga hadi mwili. Wafasiri  wengi wa Qur’ani Tukufu wanaamini kwamba jina la Adam linatoka kwa neno Adim (vumbi).

Baada ya kuumbwa kwa mwili, Mwenyezi Mungu alimpa Adam sehemu ya roho yake na hivyo akampa uhai. Uumbaji wa mwanadamu umefanywa kwa njia bora zaidi: " Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa." (aya ya 4 ya Surah at-tin) Wanadamu ndio pekee ambao katika uumbaji wao Mwenyezi Mungu amejisifu: " Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji." (Aya ya 14 ya  Surah al-Muminun)

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
AYoub
0
0
Historia ya dunia na maandiko matakatifu kiuhalisia bila kuangalia imani yoyote ile inasema Adam ndie binaadam wa kwanza kuumbwa na kuwepo duniani biblia takatifu inasema hakukua na kitu yani ilikua ni patupu tukisoma mwanzo 1:1-31 tunaona jinsi Mungu alivyo anza uumbaji wake huo ndiyo uhalisia wenyewe hauwezi kuwa wa kusadikika wala kwa wakiimani bali ndivyo ulivyo
captcha