IQNA

Harakati za Qur'ani barani Afrika

Mashindano ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu ya Mauritania yafanyika Nouakchott

21:53 - November 25, 2023
Habari ID: 3477948
NOUAKCHOTT (IQNA) – Toleo la nne la shindano la kitaifa la kuhifadhi Qur’an Tukufu na maandishi ya Kiislamu linaendelea katika mji mkuu wa Mauritania.

Mashindano hayo yalianza katika nchi hiyo ya Afrika siku ya Alhamisi kwa kushirikisha zaidi ya washindani 340 katika hatua ya awali.

Washiriki arobaini na tano watakaopata alama bora  zaidi watafanikiwa kuingia katika awamu ya mwisho, kwa mujibu wa waandaaji.

Mashindano hayo yanafanyika katika kategoria za kuhifadhi Qur'ani Tukufu, Sayansi ya Hadithi, Fiqh ya Kiislamu na Sirah ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW).

Taasisi ya Elimu ya Juu na Mafunzo ya Kiislamu ndiyo inayoandaa hafla hiyo ya Qur’ani Tukufu

Waziri wa Masuala ya Kiislamu wa Mauritania Dah Ould Sidi Ould Amar Taleb alisema katika hafla ya ufunguzi kwamba wizara yake imechukua hatua zinazohitajika kwa uratibu na wasomi wa nchi hiyo ili kuhakikisha kuwa mashindano hayo yanapangwa kwa mujibu wa viwango vilivyo wazi.

Ameongeza kuwa mashindano hayo yana nafasi muhimu katika kuendeleza mafundisho ya Qur'ani na kidini nchini humo.

Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania ni nchi iliyoko katika eneo la Maghreb magharibi mwa Afrika Kaskazini.

Idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kuwa takriban milioni 4 na takriban Wamauritania wote ni Waislamu.

Shughuli na programu za Qur'ani ni maarufu sana katika nchi hii ya Kiafrika.

 

4183787

captcha