
Umar del Pozo, Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu nchini Uhispania na Wakfu wa Msikiti wa Granada amesema kuwa suala la Palestina lilizua maswali mengi kuhusu Uislamu.
Ameliambia Shirika la Anadolu kuwa, yamkini watu wengi Ulaya wasiokuwa Waislamu wameanza kuona ukweli na kuongeza kuwa kila wiki msikiti ulioko kusini mwa mkoa wa Andalusia unashuhudia mtu mmoja au wawili wanaosilimu.
Del Pozo pia alisema kitendo cha Israel kuwaua kwa umati Wapalestina kimepelekea wengi kuwahurumia Waislamu. Amesema wengi wanaamini kuwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Palestina ni ya kidhalimu na matokeo yake ni kuwa wengi wanaanza kuuliza maswali zaidi kuhusu Uislamu.
Ameongeza kuwa, azmana irada ya Wapalestina ya kurejea makwao huku wakiendeleza mapambano dhidi ya utawala wa kikoloni wa Israel imepelekea kadhia ya Palestina iangaziwe kwa mtazamo wa kiroho. "Hivi ndivyo watu wanavyogundua Uislamu," alieleza, akiongeza kuwa mahudhurio ya maandamano ya wafuasi wa Palestina huko Granada yalikuwa makubwa.
Del Pozo alisema,."Tunaeleza kinachoendelea Palestina kwa majirani zetu Wakristo pia. Wanauliza maswali na kujaribu kujifunza zaidi kuhusu Uislamu wakati wa maandamano. Ninaweza kusema kwamba (Uislamu) ulipata umakini zaidi. Hili sio Granada pekee, Ulaya yote iko. kupaza sauti yake juu ya suala hili.”
Granada ina karibu Waislamu 37,000, ikiwa ni pamoja na Wahispania 4,000 waliosilimu na watoto wao wa kizazi cha tatu.
Uhispania ina takriban Waislamu milioni 3 wanaotoka Morocco, Pakistan, Bangladesh, Senegal, na Algeria. Wanaishi zaidi Catalonia, Valencia, Andalusia, na Madrid.
3486239