IQNA

Maisha Matakatifu (Hayat Tayyiba) /2

Kwa nini Uislamu unasisitiza kuhusu malezi bora?

19:22 - December 22, 2023
Habari ID: 3478075
IQNA – Kwa mujibu wa mafundisho ya imani ya Kiislamu, wanadamu wanaonekana kuwa ni viumbe bora na wenye uwezo wa asili unaohitaji kutambuliwa na kukuzwa; pia inashikilia kwamba mtu anaweza kupata maisha matakatifu na yenye maana ambayo yataendelea baada ya kifo.

Elimu katika Uislamu inachukuliwa kutoka mitazamo miwili. Kwanza, inategemea kanuni za falsafa, maadili, epistemolojia, na mwongozo wa vitendo kwa elimu. Kwa mfano, kulingana na Plato, elimu inapaswa kuhusisha mambo ya busara, ya kihisia, na ya hiari ili kukuza maendeleo ya binadamu.

Pili, Uislamu unachukua mtazamo wa kiuchambuzi, unaotetea majadiliano, mapitio, na upya wa dhana na nadharia katika elimu. Kwa mfano, uhusiano wa mwalimu na mwanafunzi unatazamwa kama mtiririko wa pande mbili, ambapo mwalimu akiongoza talanta kuelekea lengo la mwisho.

Huku tukikubali michango ya wanafalsafa kama Plato na Aristotle, elimu ya Kiislamu inasisitiza kwamba bila ya ukweli ulioletwa kupitia Mtume Muhammad (SAW), mwanadamu daima atakuwa mbali na elimu halisi yenye manufaa na ufanisi wa milele.

Elimu ya Kiislamu inalenga kuwatengeneza watu ambao wataweza kuwa na maisha bora duniani na akhera na wawe waja wema wa Mwenyezi Mungu. Kufikia "Hayat Tayyiba" (maisha matakatifu) ni lengo kuu na muhimu katika elimu ya Kiislamu, na maisha haya matakatifu yataendelea hata baada ya kifo.

Katika mfumo huu wa elimu, watu binafsi wanachukuliwa kuwa viumbe ambao wanapaswa kukuza uwezo wao na kuelekeza hisia zao ili kukuza nia thabiti ya kuchukua maamuzi bora, na hivyo kufikia maisha matakatifu.

Uwepo wa mshauri unachukuliwa kuwa muhimu ili kusaidia katika kudhibiti hisia na kuwaongoza watu kuelekea ukamilifu wao.

Kishikizo: maisha bora
captcha