IQNA

Mwanazuoni asisitiza kuhusu kutegemea mwongozo wa Uislamu maishani

20:04 - January 10, 2025
Habari ID: 3480024
IQNA – Mwanazuoni mwandamizi wa Kiislamu nchini Iran amesisitiza mwongozo wa kina ambao Uislamu unatoa kwa nyanja zote za maisha ya kibinafsi na kijamii.

Akizungumza katika kongamano siku ya Alhamisi, Ayatullah Mahdi Shabzendedar amesisitiza kuwa Uislamu unashughulikia mahitaji yote ya binadamu katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maisha mtu binafsi, kijamii, kiserikali, kisiasa na kitamaduni.

"Uislamu unahusika na kuongoza kila kipengele na nyanja ya maisha ya binafsi na kijamii," alisema Shabzendedar, ambaye ni katibu mkuu wa Baraza Kuu la Vyuo Vikuu vya Kiislamu (Hawza).

"Uislamu unashughulikia mahitaji yote ya binadamu katika maeneo ya kibinafsi, kijamii, kiserikali, kisiasa, kitamaduni, na mengine. Kwa hiyo, lazima tuwe na wanazuoni wenye maarifa katika nyanja zote zinazohusika na wawe na ufahamu kamili kuhusu malengo ya Mwenyezi Mungu."

Akinukuu mafundisho ya Imam Sadiq (AS), Shabzendedar alielezea umuhimu wa kutoa majibu sahihi na wazi kwa maswali na mashaka.

"Jibu linalotakiwa ni lile ambalo halijaribu tu kumshawishi upande wa pili lakini ni sahihi, halina uzushi, na halijachanganywa na uwongo. Majibu pia yanapaswa kuwa wazi na ya moja kwa moja," alieleza.

Aliendelea kusisitiza umuhimu wa kufuata masharti ya Qur’ani Tukufu na Hadith wakati wa kushughulikia mashaka.

"Katika majibu yetu, lazima tuwe na kujitolea kutoa majibu yaliyo wazi na mafupi. Jibu linapaswa kuwa na hoja kwa namna ambayo haimwachi upande mwingine akiwa amechanganyikiwa," aliongeza.

Ayatullah Shabzendedar pia alisisitiza umuhimu wa kuongeza imani ya vizazi vipya kwa Mwenyezi Mungu, akibainisha, "Kila kilichoainishwa na Mwenyezi Mungu ni lazima kutiiwa. Lazima tufanye kazi katika mambo ya Tauhudi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu ili vijana wakubali amri za Mwenyezi Mungu kama alivyosema."

Alibainisha pia kwamba kama watu na vijana wanaamini kwamba wanazuoni na viongozi wa kidini wanajali kweli kuhusu wao na sio wanaohusishwa na mambo ya kidunia, majibu yao yatakuwa na sauti kubwa. "Kama watu na vijana wanashawishika kwamba wanazuoni na viongozi wa kidini ni waaminifu na sio wanaohusishwa na mambo ya kidunia, majibu yao hakika yatawafikia wao," alisema  Ayatullah Shabzendedar.

3491402

Kishikizo: uislamu maisha
captcha