IQNA

Mwanafasihi: Lengo la Qur'ani ni kuhakikisha waumini wana maadili bora

18:24 - April 25, 2025
Habari ID: 3480590
IQNA – Mwanafasihi wa masomo ya Qur'ani amesisitiza kwamba lengo kuu la Qur'ani ni kubadilisha matendo na tabia ya waumini, si tu kusomwa tu. 

Karim Davati, mjumbe wa Kitivo cha Kikundi cha Utafiti wa Masomo ya Qur'ani, alisema kwamba Qur'ani si "kitabu cha kusomwa tu, bali ni kitabu cha athari." Matamshi yake yalitolewa wakati wa semina iliyoitwa "Usomaji wa Qur'ani: Nafasi ya Maana na Ustadi," iliyofanyika Jumatano katika Taasisi ya Masomo ya Sayansi  ya Jamii na Utamaduni. 

Davati, ambaye pia amehifadhi Qur'ani, anesisitiza kuwa Qur'ani iliteremshwa kwa hatua ili kuwezesha ufahamu  wa kina muktadha wa yaliyomo: "Hii hatua ya kuteremshwa hatua kwa hatua ni muhimu—Mtume (SAW) na Maimamu (AS) walikuwa wakiisoma mara kwa mara, wakizamisha nyoyo zao kwenye aya zake hadi watu walipoweza kuhifadhi." 

Ameashiria aya za Qur'ani ili kuonyesha usahihi wake wa Kimungu: " Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili.' (38:29). Kusoma bila kutafakari haina faida." Davati aliongeza kwamba Imam Ali (AS) aliwaonya, "Yeyote atakayetafuta mwongozo nje ya Qur'ani ataangamia." 

Mwanafasihi huyo amesisitiza kwamba madhumuni ya Qur'ani ni kubadilisha maisha ya waumini: "Lengo ni kwamba uwepo wetu wote uwe wa 'Qur'ani,' kama ambavyo tabia ya Mtume (SAW) ilidhihirisha kikamilifu. Imam Ali (AS) anaitwa 'Qur'ani Inayozungumza' kwa sababu matendo yake yalionyesha kila fundisho la Qur'ani." 

Davati alielezea njia za kushirikiana na Qur'ani, ikijumuisha tilawah (usomaji) na tarteel (usomaji wa taratibu), akitaja aya " Au izidishe - na soma Qur´ani kwa utaratibu na utungo " (73:4). Amebainisha kuwa Mtume (SAW) alikuwa akisoma mara kwa mara ili kuhakikisha kuhifadhi na kusambazwa kwa Qur'ani. 

Aidha amesema kuna mwelekeo wa sanaa katika usomaji, Davati alifafanua: "Usomaji si sanaa tu, bali sanaa inaongeza athari zake. Mtume (SAW) alibadilisha usomaji wake kulingana na uwezo wa wasikilizaji wake, akiwavutia wasikilizaji." 

3492830

captcha