IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran watangazwa

19:07 - February 21, 2024
Habari ID: 3478392
IQNA-Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalimalizika Jumatano huku washindi wakitunukiwa zawadi.

Sherehe za kufunga mashindano hayo ya kimataifa zilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Tehran kwa kushirikisha washiriki, waandaaji na maafisa wakuu wa Iran akiwemo Rais Ebrahim Raisi .

Jopo la majaji lilimtangaza Hadi Esfidani wa Iran kuwa mshindi wa kitengo cha Qiraa kwa wanaume akifuatiwa na Mustafa Branun kutoka Thailand na Mustafa Ali kutoka Uholanzi alifuata.

Katika kitengo cha Kuhifadhi Qur'ani Tukufu kwa  wanaume, Omidreza Rahimi kutoka Iran alishinda nafasi ya kwanza. Burhaneddin Rahimov kutoka Urusi na Khuzaifa Quraishi kutoka Algeria walishika nafasi za pili na za tatu kwa taratibu.

Katika kategoria ya wanawake ya kuhifadhi Qur'ani, Roya Fazaeli kutoka Iran alishika nafasi ya kwanza. Maimonah Badeqi kutoka Nigeria na Nouria Jurian Erqa kutoka Indonesia walifuata. Halikadhalika pia kulikuwa na mashindano ya wanafunzi wa shule katika mashindano hayo.

Adeleh Sheikhi wa Iran alitajwa kuwa mshindi wa kwanza katika kitengo cha wanawake cha usomaji wa Tarteel. Atiqeh Sahimi kutoka Singapore na Doa al-Saeed kutoka Iraqi walifuata kwa taratibu

Mashidano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalianza siku ya Alkhamisi na kuwavutia wapenzi wa Qur'ani kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 110 walijiandikisha kwa ajili ya Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran, lakini ni washiriki 69 tu kutoka nchi 40  ndio waliofanikiwa kuingia katika duru ya mwisho baada ya mchakato mkali wa kuchujwa.

3487293

Habari zinazohusiana
captcha