IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

Siku ya 4 ya Awamu ya 40 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

20:45 - February 20, 2024
Habari ID: 3478384
IQNA - Katika siku ya nne Awamu ya 40 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran, makari na wahifadhi kadhaa kutoka mataifa tofauti walipanda jukwaani.

Mashindano hayo yaliendelea Jumatatu asubuhi na alasiri.

Sehemu ya wanawake ilimalizika asubuhi baada ya siku tatu za mashindano katika kategoria za usomaji wa Tarteel na kuhifadhi Qur'ani. Washiriki sasa wanasubiri matokeo yatakayotangazwa katika hafla ya kufunga Jumatano.

Mashindano ya wanaume ambayo yalifanyika mchana na kudumu kwa saa kadhaa yalikuwa na maqarii wanne na wahifadhi wanne wa Qur'ani Tukufu waliopanda jukwani.

Wawakilishi kutoka Iraq, Malaysia, Uholanzi na Singapore waliwasilisha maonyesho yao katika kategoria ya qiraa ya Tahqiq.

Abdullah Zahir Hadi kutoka Iraq alisoma aya za 165-170 za Surah Al-Baqarah.

Katika kategoria ya kukariri wanaume, wawakilishi kutoka Iran, Tunisia, Algeria, na Syria walipanda jukwaani na unaweza kutazama waliovyosoma kwa kubonyeza hapa.

Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalianza Alkhamisi mjini Tehran katika sherehe iliyohudhuriwa viongozi wa Iran na wapenda Qur'ani kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Kwa mujibu wa waandaaji hao, zaidi ya wawakilishi wa nchi 110 walijiandikisha kushiriki mashindano hayo na walioingia fainali ni washiriki 69 kutoka nchi 40 zilifuzu kwa awamu ya mwisho baada ya mchujo wa awali.

Mashindano hayo yanatazamiwa kuendelea hadi Jumanne, Februari 20, na washindi watatangazwa na kutunukiwa katika hafla ya kufunga Jumatano, Februari 21.

3487266

Habari zinazohusiana
captcha