IQNA

Ugaidi

Makumi ya Waislamu wauawa katika hujuma msikitini Burkina Faso

16:59 - February 27, 2024
Habari ID: 3478419
IQNA - Shambulio dhidi ya msikiti mashariki mwa Burkina Faso liliua makumi ya Waislamu siku ambayo a shambulio lingine baya dhidi ya Wakatoliki waliokuwa kanisani.

"Watu wenye silaha walishambulia msikiti mmoja huko Natiaboani Jumapili mwendo wa saa kumi na moja asubuhi, na kusababisha makumi kadhaa kuuawa," afisa wa usalama alidokeza siku ya Jumatatu.

"Wahasiriwa wote walikuwa Waislamu, wengi wao wanaume" ambao walikuja kwa sala ya Alfajiri, mkazi wa eneo hilo alisema kwa simu.

Chanzo kingine cha habari kilisema, “Magaidi waliingia mjini mapema asubuhi. Waliuzunguka msikiti na kuwapiga risasi waumini waliokuwa wamekusanyika hapo kwa ajili ya sala ya kwanza ya siku hiyo. Wengi wao walipigwa risasi, akiwemo kiongozi wa kidini katika eneo hilo.”

Wanajeshi na wanachama wa Kikosi cha Kujitolea cha Kulinda Nchi (VDP), kikosi cha kiraia kinachounga mkono jeshi, pia walilengwa "na washambuliaji waliokuja kwa wingi", chanzo kilisema.

Maafisa wa usalama wanasema lilikuwa "shambulio kubwa" kulingana na idadi ya washambuliaji, ambao pia walifanya uharibifu mkubwa.

Natiaboani ni jamii ya vijijini takriban kilomita 60 (maili 37) kusini mwa Fada N'Gourma, mji mkuu katika eneo la mashariki la Burkin Faso, ambao umekuwa ukishuhudia mashambulizi ya mara kwa mara ya makundi yenye silaha tangu 2018. Eneo hilo liko karibu na mpaka na Benin na Togo.

Siku ya shambulio dhidi ya msikiti huo, takriban raia 15 waliuawa na wengine wawili kujeruhiwa katika shambulio dhidi ya kanisa katoliki wakati wa misa ya Jumapili kaskazini mwa Burkina Faso, afisa mkuu wa kanisa hilo alisema.

Jean-Pierre Sawadogo, kasisi wa dayosisi ya Dori, alisema katika taarifa yake kwamba "shambulio la kigaidi" lilifanyika katika kijiji cha Essakane wakati watu walikuwa wamekusanyika kwa sala ya Jumapili.

Kijiji cha Essakane kiko katika kile kinachojulikana kama ukanda wa "mipaka mitatu" kaskazini mashariki mwa nchi, karibu na mipaka ya kawaida ya Burkina Faso, Mali na Niger.

Kwa mujibu wa Mradi wa Kudhibiti Migogoro ya Mahali na Tukio (ACLED), takriban watu 20,000 nchini Burkina Faso wameuawa katika ghasia zilizosambaa kutoka Mali ambapo zilianza mwaka 2012. Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu milioni mbili wameyakimbia makazi yao.

Vikosi kadhaa vya kijeshi pia vilishambuliwa siku ya Jumapili katika maeneo tofauti ya mashariki na kaskazini mwa Burkina Faso. Kulingana na vyanzo vya usalama, "magaidi" mia kadhaa "wameuawa" katika operesheni za kujibu mashambulizi.

Kwa muongo mmoja sasa, Burkina Faso imekuwa ikikabiliana na machafuko yanayohusishwa na makundi ya kigaidi ya al-Qaeda na Daesh/ISIS.

Wanajeshi wa Ufaransa walikuwa nchini Burkina Faso kwa zaidi ya miaka kumi kwa kisingizio cha kuisaidia nchi hiyo kupambana na ugaidi. Hata hivyo, magaidi walipata nguvu zaidi wakati wa uwepo wa wanajeshi wa Ufaransa nchini humo.

Kutokana na hali hiyo, mwaka jana serikali ya kijeshi iliamuru wanajeshi wa Ufaransa kuondoka nchini mara moja. Russia sasa inaisaidia Burkina Faso katika mapambano yake dhidi ya ugaidi na kuna matumaini kuwa mashambulizi ya kigaidi yatapungua kwa kiasi kikubwa katika miezi ijayo.

3487348

captcha