IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

Mafanikio ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran ni natija ya juhudi za pamoja

17:39 - February 27, 2024
Habari ID: 3478423
IQNA - Mafanikio ya katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran ni matokeo ya juhudi za pamoja katika uwanja wa shughuli za Qur'ani nchini, afisa mwandamizi amesema.

Hujjatul Islam Seyed Mehdi Khamoushi aliyasema hayo katika mahojiano yake na Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), wiki moja baada ya kumalizika kwa Awamu ya 40 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran mjini Tehran.

Amesema tukio hilo la kimataifa la Qur'ani lina mizizi ya kihistoria katika ulimwengu wa Kiislamu.

Akiangazia vipengele maalum vya mashindano hayo, alisema yameandaliwa kwa miaka 40 mfululizo bila kusitishwa.

Ameongeza kuwa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran yaliendelea hata  wakati wa janga la coronavirus wakati nchi nyingi zilisimamisha mashindano yao.

Sifa nyingine ni idadi ya washindani, mwanazuoni huyo  alisema, akibainisha kuwa idadi ya wahifadhi na wasomaji Qur'ani Tukufu kutoka zaidi ya nchi 110 walishiriki katika mashindano ya mwaka huu.

Baada ya tathmini za awali na kufanya duru ya kwanza, washiriki 90 kutoka nchi 44 walifuzu katika fainali alisema.

Kushiriki kwa idadi hiyo kubwa ya wanaharakati wa Qur'ani katika mashindano ya Iran kumeyafanya kuwa mashindano muhimu ya Qur'ani katika ulimwengu wa Kiislamu, ambayo ni mafanikio ambayo yanapaswa kulindwa, aliongeza.

Hujjatul Islam Khamoushi pia aliangazia mchakato wa mtandaoni wa jopo la majaji  katika mashindano hayo pia mafanikio mengine katika toleo la mwaka huu.

Ubora wa hukumu katika mashindano ya Qur'ani la Iran pia ulikuwa wa juu sana, kwa mujibu wa msomi huyo.

Hatua nyingine kubwa ni kuanzisha suala la kutoa mafunzo kwa washiriki, alisema, akibainisha kuwa washiriki walipewa mafunzo kabla ya kuwasili Iran na hata wakiwa, jambo ambalo liliinua kiwango cha mashindano na kukaribishwa sana.

Hujjatul Islam Khamoushi aliendelea kusema kuwa, Qur'ani Tukufu ni nguzo ya umoja katika ulimwengu wa Kiislamu, akisisitiza haja ya Iran kuwa mshika bendera wa shughuli za Qur'ani katika nyanja za qiraa, kuhifadhi na ufahamu wa aya Qur'ani. Amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ndiyo mshika bendera wa umoja wa Waislamu.

Hujjatul Islam Khamoushi ni Mkuu wa Shirika la Masuala ya Wakfu na Misaada la Iran, ambalo huandaa mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani Iran.

Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yalifanyika mjini Tehran mapema mwezi huu yakiwa na kauli mbiu ya "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja, Kitabu cha Mapambano (Muqawama)".

Washindi wa kategoria tofauti katika sehemu za wanaume na wanawake walitajwa na kutunukiwa katika hafla ya kufunga iliyofanyika Jumatano jioni, Februari 21.

3487354

Habari zinazohusiana
captcha