IQNA

Qur'ani Tukufu barani Afrika

Usomaji wa Qur'ani wenye mvuto wa watoto wa Kiafrika + video

14:55 - February 28, 2024
Habari ID: 3478425
IQNA-Video iliyosambazwa na mtalii wa Morocco, ambapo watoto wa Kiafrika wanasoma aya za Sura Maryam kwa njia nzuri na ya kipekee, imewavutia wengi katika mitandao ya kijamii.

Yeni Shafaq, mtalii wa Morocco aliyesambaza video hii ameambatanisha maandishi yasemayo: "Wakati wa safari yangu katika nchi moja ya Afrika, nilikuwa nikipita kwenye kijiji kimoja kidogo na nikasikia sauti nzuri wakati wa usiku, nikaenda kuitafuta na baada ya muda niliona watoto wakiwa wanasoma aya za Quran Tukufu. Katika video iliyosambazwa, watoto hao wanasikika wakisoma Sura Maryam aya ya 30-34.

(Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai, Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu. Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai. Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka.

4202312

captcha