IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema, kwa kuzingatia Aya za Qur'ani Tukufu na kumbukumbu ya jina lililobarikiwa la Nabii Ibrahim (AS), ibada ya Hija ya mwaka huu inapaswa kuwa zaidi ya Hija ya kila mwaka, na inabidi iwe Hija na kutangazwa kujitenga au kujibari na adui wa Waislamu, Mzayuni mtenda uhalifu na wafuasi wake wa nchi za Marekani, Uingereza na Wamagharibi kwa ujumla.
Ayatullah Khamenei aliyasema hayo Mei 6 jijini Tehran alipohutubia kikao cha maafisa na wasimamizi wa msafara wa mahujaji wa Iran wanaoelekea katika ardhi tukufu kwa ajili ya ibada ya Hija.
