IQNA

Mkenya aenda Hija baada ya kuuza viungo vya chakula miaka 15

13:16 - September 23, 2015
Habari ID: 3366740
Kuhiji kwa mara ya kwanza ni ndoto iliyotimia kwa Abdi Mohammad, Mwislamu kutoka Kenya ambaye amekuwa akiuza viungo vya chakula kwa muda wa miaka 15 ili aweze kuchanga pesa za kumuwezesha kutimiza faradhi ya Hija katika mji mtakatifu wa Makkah.

"Nilinuia kuwa nitajitahidi kutekeleza Ibada ya Hija kabla ya kuagad dunia," Abdi Mohammad, 62 ameliambia shirika la habari la Anadolu.
"Nimekuwa nikiuza viungo vya chakula katika mtaa wa Eastleigh, Nairobi, kwa muda wa miaka 15 sasa. Biashara haikuwa nzuri wakati wote, kuna baadhi ya siku nililala njaa, lakini daima niliweka akiba katika akaunti maalumu kwa ajili ya safari hii."
"Hija ni nguzo tano ya  Uislamu, na nina yakini kuwa nikitekeleza ibada hii, Allah atanimiminia baraka zake kwani Yeye Ndie Mkubwa Zaidi," aliongeza.
Mohammad anatakeelza ibada ya Hija mwaka huu katika Msafara wa Mahujaji wa Kenya wenye mahijaji takribani 4,500.
Mohammad amesema kuna watu anaowajua walio juu ya umri wa miaka 70 na wangali wanaweka akiba kwa ajili ya safari ya Hija.
"Serikali inapaswa kutusaidia hasa wazee miongoni mwetu waweze kutekeleza ibada ya Hija kwa kuzungumza na Wasaudi waongeze nafasi wanazotoa kwa wale wanaotaka kuelekea Makka kuhiji."
Shariff Hussein, Naibu Mkuu wa Msafara wa Hija Kenya ametoa  wito kwa serikali ya Saudia kuongeza nafasi 500 katika msafara wa hija wa Kenya kutokana na ongezeko la kasi la Waislamu nchini humo.../mh

3366660

captcha