Sheikh Naim Qassem ameyasema hayo katika kumbukumbu ya kwanza ya kuuliwa shahidi kwa Fawad Shukr mmoja wa makamanda mashuhuri wa harakati hiyo ya Kiislamu.
Aidha amesisitiza kuwa, harakati hiyo ya muqawama kamwe halitakubali kukabidhi silaha zake kwa Israel.
Katibu Mkuu wa Hizbullah amesisitiza kuwa, silaha hizo ni muhimu kwa ajili ya kulindai mamlaka ya kitaifa ya Lebanon mbele ya uvamizi wa utawala wa Tel Aviv.
Katika hotuba yake iliyotangazwa na televisheni kutoka mji mkuu wa Lebanon, Beirut, Jumatano ameongeza kuwa wale wanaotaka kunyang'anywa silaha za Hizbullah wanatumikia maslahi ya Israel, na wanajifungamanisha na adui Mzayuni.
Amelaani juhudi zinazofanyika ili kupokonya silaha za Hizbullah akizitaja kuwa ni kujisalimisha kwa Israel, na kusisitiza haja ya umoja wa kitaifa, ulinzi na ujenzi mpya.
"Wito wowote wa kutupokonya silaha una maana ya kudhoofisha nguvu ya Lebanon. Kuipokonya silaha Hizbullah kutaiwezesha Israel kupanua uvamizi wake na kudhibiti ardhi ya Lebanon," amesema Sheikh Qassem.
Ameonya kwamba Lebanon inakabiliwa na tishio - sio tu kutoka kwa Israel, bali pia kutoka kwa Marekani na kundi la kigaidi la Daesh, chini ya kivuli cha "Mashariki ya Kati Mpya."
Sheikh Naim Qassem amesisitiza kwamba adui Israel hataishia katika kukalia kwa mabavu maeneo matano muhimu kusini mwa Lebanon, na anasubiri kupokonywa silaha na Hizbullah ili kupanua shughuli zake za ujenzi wa vitongoji haramu.
4297339