Ayatullah Alireza Arafi, mkuu wa vyuo vikuu vya Kiislamu nchini Iran, ametuma barua kwa viongozi 26 mashuhuri wa kidini—akiwemo
Miongoni mwa waliopokea barua hiyo ni Papa Leo wa XIV, Sheikh Ahmed El-Tayyeb, Imamu Mkuu wa Al-Azhar, pamoja na Sheikh Salih bin Abdullah al-Humaid, kiongozi mwandamizi wa kidini kutoka Saudi Arabia ambaye pia ni Imamu wa Msikiti Mtakatifu wa Makka (Masjid al-Haram). Pia barua hiyo imemfikia Sheikh Ali al-Qaradaghi kutoka Jumuiya ya Kimataifa ya Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS). Wanazuoni wa kidini wa Pakistan, Indonesia, na India pia wamepokea barua hiyo muhimu.
akihimiza hatua za dharura zichukuliwe kuvunja mzingiro wa Israel na kukomesha "uhalifu wa kivita" unaofanyika Gaza.
“Kwa moyo unaoumia kwa sababu ya uhalifu wa kivita wa Wazayuni na roho iliyojawa na udugu wa Kiislamu, ninaandika barua hii,” amesema Ayatullah Arafi.
Amelaani "dhuluma dhidi ya Gaza" akisema siyo tu mgogoro wa kisiasa bali ni "mtihani wa kiroho" kwa dhamira ya dunia nzima, na akawataka wanazuoni "kukabiliana na madhalimu" na kushinikiza serikali kuchukua hatua.
Wito wake unakuja wakati Wizara ya Afya ya Gaza imeripoti kuwa Wapalestina wengine 10 wamekufa kwa njaa siku ya Jumatano, na kufikisha idadi ya vifo vya njaa na utapiamlo hadi 111 tangu Oktoba 2023—wakiwemo watoto 21 walio chini ya miaka mitano. Mashambulizi ya Israel yameua Wapalestina wengine 100 ndani ya saa 24, wakiwemo watu 34 waliokuwa wakitafuta msaada. Umoja wa Mataifa unasema kuwa wanajeshi wa Israel wamewapiga risasi zaidi ya raia 1,000 karibu na maeneo ya misaada tangu Mei.
Katika barua hiyo, Arafi alieleza kuwa utawala wa Israel unakandamiza Gaza kimakusudi, huku mashirika ya UN yakiripoti kuzuiliwa kupeleka chakula kwa miezi kadhaa. “Njaa ya watoto Waislamu haina kisingizio mbele ya Mwenyezi Mungu,” aliandika, akisisitiza ulazima wa msaada wa haraka na kupendekeza mikutano ya wanazuoni wa kimataifa ili kuratibu juhudi za misaada.
Kwa sasa, msaada mdogo tu ndio unaingia Gaza kupitia Mfuko wa Misaada ya Kibinadamu wa Gaza (GHF), unaoungwa mkono na Marekani, ambao unapingwa na baadhi ya wahisani.
Hivi karibuni, mashirika 111 ya misaada—ikiwemo Mercy Corps na Refugees International—yameonya kuhusu “njaa ya pamoja” huku shehena za misaada zikiendelea kuoza mipakani mwa Gaza.
“Umma wa Kiislamu lazima uchukue hatua za msingi,” alisisitiza Arafi, akiapa kuwa Iran “itaendelea kutoa sauti kubwa ya uungaji mkono” kwa watu wa Gaza.
Wito wake unaendana na ule wa maafisa wa UN wanaotaka msaada kufikishwa bila vikwazo, ambapo Ross Smith wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani alisema: “Hatuhitaji wapiganaji karibu na misafara yetu ya misaada.”
Israel ilianzisha mashambulizi yake ya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 7, 2023. Tangu wakati huo, zaidi ya Wapalestina zaidi ya 58,000 wameuawa shahidi, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza.
3493970