IQNA

Turathi za Kiislamu

Mkuu wa Al-Azhar atembelea Msikiti wa Sayyida Zainab (SA) jijini Cairo

22:35 - May 15, 2024
Habari ID: 3478828
IQNA – Sheikh Ahmed al-Tayyeb, Imamu wa Al-Azhar, alitembelea Msikiti wa Sayyida Zainab (SA mjini Cairo siku moja baada ya kufunguliwa tena.

Sheikh Al-Tayyeb alikaribishwa na Waziri wa Wakfu Mohamed Mukhtar Gomma na baadhi ya maafisa wengine katika ziara hiyo.

Alizunguka sehemu mbalimbali za msikiti huo na kuswali.

Sheikh Gomma alimweleza kuhusu mchakato wa ukarabati na katika msikiti huo wa kihistoria

Sheikh wa Al-Azhar alishukuru wizara na juhudi za serikali za kukarabati na  misikiti ya kale na maeneo ya turathi nchini.

Msikiti wa Sayyida Zainab (SA) ulifunguliwa tena katika sherehe siku ya Jumapili baada ya kumalizika kwa kazi za ukarabati.

Ni moja ya misikiti mikubwa na maarufu katika mji mkuu wa Misri.

Kwa mujibu wa baadhi ya wanahistoria wa Kiislamu, Bibi Zainab (SA), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), amezikwa hapo.

Msikiti huo una nafasi maalum na muhimu katika historia na utamaduni wa mji huo na umekuwa kituo kikuu cha duru za Qur'ani na mikusanyiko ya kidini kwa karne nyingi.

Al-Azhar Chief Visits Sayyida Zaynab Mosque in Cairo

Al-Azhar Chief Visits Sayyida Zaynab Mosque in Cairo

Al-Azhar Chief Visits Sayyida Zaynab Mosque in Cairo

Al-Azhar Chief Visits Sayyida Zaynab Mosque in Cairo

4215674

 

Habari zinazohusiana
captcha