IQNA

12:50 - April 06, 2020
Habari ID: 3472637
TEHRAN (IQNA)- Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri kimetoa wito wa kusitishwa vita na umwagaji damu kote duiani.

Katika taarifa ya Aprili 5 kwa munasaba wa Siku ya Kimataifa ya Dhamira, Al-Azhar imesema sikuu hii ni wakati muafaka wa kustawisha na kuimarisha mshikamano, ushirikiano na udugu wa watu wote.

Taarifa hiyo imesema Siku ya Kimataifa ya Dhamira ni kengele ya hatari kila mwaka  ya kuhutubi jamii ya mwandamu kuhusu kuwarejeshea watu haki zao, kuokoa maisha, na kusitisha umwagaji damu.

Umoja wa Mataifa uliitangaza Aprili 5 kuwa Siku ya Kimataifa ya Dhamira ili kuandaa mazingira ya uthabiti, usalama, urafiki na urafiki wa mataifa yote kwa msingi wa haki za binadamu na uhuru bila kujali rangu, dini, lugha au jinsia.

3889489

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: