IQNA

Harakati za Qur'ani

Msikiti wa Imam Hussein (AS) jijini Cairo waandaa vikao vya Qur'ani Tukufu

17:31 - August 27, 2024
Habari ID: 3479335
IQNA – Kikao cha usomaji Qur'ani Tukufu na  Ibtihal kilifanyika katika Msikiti wa Imam Hussein (AS) huko Cairo, mji mkuu wa Misri.

Baadhi ya maqari maarufu, akiwemo Ahmed Ahmed Nuaina, Mahmoud al-Khisht, Abdul Fattah al-Taruti, Yasir al-Sharqawi, Taha al-Numani, Ahmed Tamim al-Maraqi, na Mahir al-Farmawi walisoma Qur'ani katika halqa hiyo.

Waziri wa Wakfu Misri f Osama El-Azhari na washiriki katika toleo la 35 la mkutano wa kimataifa uliopewa jina la "Wajibu wa Mwanamke katika Kujenga Uelewa" walihudhuria tukio hilo la Qur'ani, tovuti ya Ad-Dustur iliripoti.

Programu ya usomaji wa Qur'ani na Ibtihal ilikuwa ikifanyika katika eneo la mkutano katika toleo lililopita, lakini, kwa mujibu wa waziri wa wakfu, iliamuliwa kupangwa msikitini hapo ili wageni wanufaike na anga yake ya kiroho.

Mkutano huo wa kimataifa umevutia idadi kubwa ya wanazuoni kutoka Misri na nchi nyingine za ulimwengu wa Kiislamu, El-Azhari alibainisha.

Akigusia mada ya kongamano hilo, Waziri huyo ameashiria nafasi ya mwanamke katika kuelimisha jamii na kusema wanawake wakiwemo Ahl-ul-Bayt (AS) wa Mtume Mtukufu (SAW) wamekuwa na nafasi kubwa katika historia ya Uislamu.

 

3489655

captcha