IQNA

Tarjuma ya Kiswahili ya Qurani katika Maonyesho ya Vitabu Cairo

22:15 - July 12, 2021
Habari ID: 3474093
TEHRAN (IQNA) – Tarjuma za Qurani Tukufu kwa lugha za Kiswahili na Kiindonesia ni kati ya vitaby vipya ambavyo vimewasilishwa katika Maoneysho ya Kimataifa ya Vitabu ya Cairo.

Hayo yamedokezwa na Waziri wa Wakfu Misri Sheikh Mokhtar Gomaa ambaye amesema wanaotembelea maonyesho hayo wanaweza kununua tarjuma hizo kwa bei nafuu ambayo imepunguzwa kwa asilimia 50.

Sheikh Gomaa amesema kuchapisha tarjama za Qur’ani Tukufu ni katika majukumu ya wizara hiyo ya kueneza fikra za Kiislamu zenye mitazamo ya wastani ili kukabiliana na wenye misimamo mikali.

Maoneyesho ya 52 ya Vitabu ya Cairo yalianza Juni 30 na yataendelea hadi Julai 15.

3983165

captcha