IQNA

Utamaduni

Qur’ani Tukufu: Kitabu kinachouzwa kwa wingi katika Maoynesho ya Vitabu Cairo

18:50 - February 05, 2024
Habari ID: 3478306
IQNA - Waandaaji wa toleo la 55 la Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Cairo wanasema Misahafu au nakala za Qur’ani Tukufu ni vitabu vinavyouzwa kwa wingi zaidi katika hafla hiyo ya kitamaduni.

Maonyesho hayo ya vitabu yanaendelea katika mji mkuu wa Misri kwa kushirikisha wachapishaji 1,200 kutoka Misri na nyingine 70.

Kulingana na waandaaji, wageni wanaotembelea maonyesho wamekaribisha kwa kiasi kikubwa mabanda yanayouza Quran.

Hadi sasa zaidi ya watu milioni 2.8 wametembelea maonyesho ya vitabu katika Kituo cha Maonyesho cha Kimataifa cha Cairo.

Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Cairo ni maonyesho makubwa na kongwe zaidi ya vitabu katika ulimwengu wa Kiarabu, yanayofanyika kila mwaka kuanzia wiki ya mwisho ya Januari huko Cairo, Misri.

Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Cairo yamepokea idadi  kubwa zaidi ya wageni iliyovunja rekodi, ambapo zaidi ya watu milioni 3.5 wametembelea hafla hiyo.

Maonyesho hayo, yaliyozinduliwa Januari 25 na kuendelea hadi Februari 6, ni­­­ moja ya hafla kuu za kitamaduni nchini humo, huleta pamoja wadau wa sanaa, fasihi na mashairi.

3487081

captcha