IQNA

Qur'ani Tukufu

Al-Azhar yachapisha ripoti kuhusu Shughuli Zake za Qurani za 2023

16:42 - January 03, 2024
Habari ID: 3478139
IQNA - Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kilichapisha ripoti inayofafanua shughuli zake za Qur'ani mnamo 2023.

Kwa mujibu wa ripoti, kituo hicho kilizindua zaidi ya kozi 1,000 za Qur'ani Tukufu kwa watoto katika majimbo tofauti ya nchi hiyo.

Pia iliandaa madarasa 11,823 ya kufundisha Qur'ani Tukufu mtandaoni pamoja na programu 21,740 za kila wiki za usomaji na kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa zaidi ya wakufunzi 164,000 walifundisha Qur'ani Tukufu katika vituo vya Qur'ani Tukufu kwa watoto vinavyohusiana na Al-Azhar.

Idadi ya wanaofundisha Quran kwa watu wazima katika vituo vya Qur'ani Tukufu vilivyounganishwa na Al-Azhar ilikuwa 27,343.

Kuchapisha vitabu vya Qur'ani, kufanya mashindano ya Qur'ani na kuandaa kongamano na makongamano ya Qur'ani ni miongoni mwa shughuli nyingine kuu za Qur'ani za kituo hicho mwaka jana.

Pia iliendesha programu za elimu katika nyanja za sayansi na Hadithi za Qur'ani.

Ripoti ya Al-Azhar iliendelea kubainisha kwamba kituo hicho kiliandaa vikao na makongamano kadhaa kwa ajili ya kuunga mkono kadhia ya Palestina, likiwemo moja lililokuwa na mijadala kuhusu hadhi ya mji mtakatifu wa Quds katika Uislamu.

Al-Azhar ni msikiti wa kihistoria na kituo cha Kiislamu huko Cairo, mji mkuu wa Misri.

Khalifa wa Fatimiyya aliagiza ujenzi wake kwa jiji kuu jipya lililoanzishwa mwaka wa 970 W.K. Ulikuwa msikiti wa kwanza kuanzishwa katika jiji hilo.

3486662

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu al azhar
captcha