IQNA

Taarifa ya Al Azhar kuhusu uvumi wa kuwadia mwisho wa dunia

12:47 - July 02, 2020
Habari ID: 3472921
TEHRAN (IQNA) - Kituo cha Kimataifa cha Fatwa katika Chuo Kikuu cha Al Azhar nchini Misri kimetoa taarifa kuhusu uvumizi unaoenezwa kuwa umewadia mwisho wa dunia au qiyamah.

Kwa mujibu wa tovuti ya arabic.rt.com/ , taarifa hiyo ya Al Azhar imesema: "Kumeeneza uvumi sana kuhusu kuwadia zama  za mwisho (Youm al Saat) na hata makala zimeandikwa kuhusu kuwadia siku hii. Hayo ni kinyume cha Kitabu cha Allah SWT na Sunna ya Mtume SAW."

Aidha Taarifa hiyo imesema: "Allah SWT amefanya kuwa siri yake wakati wa kuwadia Siku ya Qiyamah ili kuweza kutafautisha baina ya watenda mema na watenda dhambi na pia waja wema nao wachukue tahadhari kutokana na imani kuwa siku ya qiyama inaweza kutokea wakati wowote ule na hivyo wajibidiishe kutenga amali njema huku wakiwa na hamu zaidi ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu."

Kituo hicho kimetahadharisha kuwa uvumi unakiuka akili na mafundisho ya kidini.

3908164

captcha