IQNA

Sheikh Zakzaky wa Nigeria akutana na mwanazuoni mwandamizi wa Iraq jijini Najaf

16:52 - May 19, 2024
Habari ID: 3478851
IQNA - Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria, amefanya mazungumzo na Ayatullah Sheikh Mohammad Yaqubi, Marjaa Taqlid nchini Iraq, katika mji mtakatifu wa Najaf

Katika kikao hiki, Ayatullah Yaqubi amesisitiza ulazima wa kufanya juhudi na kukusanya rasilimali ili kuleta sauti ya Uislamu wa kweli duniani na kukuza fahari ya mafundisho Ahl-ul-Bayt (AS).

Ameongeza kuwa changamoto zinazoukabili Ummah wa Kiislamu hivi leo zinapaswa kushughulikiwa kwa kutumia njia madhubuti na kwa kuzingatia mahitaji na masharti ya kisasa.

Ayatullah Yaqubi pia amemsifu Sheikh Zakzaky kwa uthabiti na ustahimilivu wake katika kukabiliana na matatizo na misiba.

Alitumai kwamba uenezaji wa Sheikh Zakzaky wa mafundisho ya Ahl-ul-Bayt (AS) hautabakia Nigeria pekee bali utaenea Afrika nzima.

Alieleza zaidi kuanzisha na kuendeleza seminari za Kiislamu katika nchi za Kiafrika kuwa ni jambo la lazima.

Sheikh Zakzaky katika mkutano huu ameshukuru chanzo cha kuigwa kwa uungaji mkono wake kwa wanafunzi wa seminari za Kiafrika na msisitizo wake katika kueneza dini na mwamko wa Umma.

Vile vile ameashiria kuenea kwa Uislamu wa Shia barani Afrika na kusema katika miongo kadhaa iliyopita, mamilioni ya watu katika nchi za Kiafrika wameikumbatia shule ya Ahl-ul-Bayt (AS)

4216379.

Kishikizo: zakzaky
captcha