IQNA

Mwakilishi wa Ayatullah Khamenei akutana na Sheikh Zakzaky wa Nigeria, wajadili matukio ya ulimwengu wa Kiislamu

19:13 - September 04, 2024
Habari ID: 3479384
IQNA - Sheikh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, alikutana na mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei nchini Iraq.

Katika mkutano huo, uliofanyika katika mji mtakatifu wa Najaf, Sheikh Zakzaky na Ayatullah Seyed Mojtaba Hosseini walizungumza kuhusu matukio na maendeleo ya sasa katika ulimwengu wa Kiislamu.

Wanazuoni hao wawili wakuu pia walijadili masuala yanayohusiana na bara la Afrika.

Katika mazungumzo hayo, Sheikh Zakzaky alishukuru shughuli za ofisi ya mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu nchini Iraq.

Ujumbe wa wanazuoni wa Nigeria na Afrika, wanachuo wa vyuo vya kidinina watu mashuhuri wa kidini waliandamana na Sheikh Zakzaky katika mkusanyiko huo.

Ayatullah Hosseini pia alizungumza na wanafunzi wa Kiafrika wa seminari au Hauza wanaosoma katika Seminari ya Kiislamu ya Najaf waliohudhuria mkutano huo.

Sheikh Zakzaky, ambaye ni mkuu wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria (IMN), na mkewe walikuwa gerezani nchini Nigeria kwa miaka sita kwa tuhuma za uongo kabla ya kuachiliwa huru Julai 2021 kufuatia harakati za zilizoendelea bila kusita za Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Nigeria. na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu.

 

4234719

captcha